• Isikupite Hii

  April 10, 2015

  SOMO: JINSI YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU.


  Swali hili limekuwa likiulizwa na watu wasiohesabika katika vizazi vingi. Samweli aliisikia sauti ya Mungu, lakini hakuitambua hadi alipoamuriwa na Eli (Samweli 3: 1-10). Mungu Alijifunua Dhahili kabisa Kwa Gideoni, Lakini Bado Gideoni alikuwa na mashaka hadi akaomba ishara kutoka kwa Mungu,  na sio mara moja bali ni mara tatu (Waamuzi 6:17-22, 36-40). 

  Wakati tunaisikiza sauti ya Mungu, tutawezaje kutambua kwamba ni yeye anazungumza? Kwanza Kabisa sisi tuna kitu ambacho Gideoni na Samweli hawakuwa nacho. Tuna Bibilia iliyo kamilika, iliyo na pumzi ya Mungu, tusome, tujifunze, na kuitafakari. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16-17). Tukiwa na swali kuhusu jambo fulani au uamuzi katika maisha yetu, tuakikishe kwanza Bibilia inasema nini kuhusu hilo swali. Mungu hawezi kutuongoza, au kutuelekeza kinyume na yale alioyaandika na kuyahaidi katika neno lake (Tito 1:2).

  Pili, ili tusikie satu ya Mungu lazima tuitambue. Yesu alisema, “Kondoo wangu waisikia satu yangu; nami nawajua, nao wanifuata” (Yohana 10:27). Walio wake huisikia sauti yake, wale ambao wameokolewa kwa neema yake kupitia kwa imani katika Kristo Yesu. Hawa ndio kondoo ambao wanaisikia na kuitambua sauti yake, kwa sababu wanamjua kama mchungaji wao na wanaijua sauti yake. Kama tunataka kuitambua sauti yake, lazima tuje kwake.

  Tatu, tunasikia sauti yake wakati tunachukua muda wetu katika maombi, kujifunza na kutafakari neno lake. Tunapotumia muda wetu katika kusoma neno na kukaa katika uwepo wa Mungu, ndivyo inavyokuwa rahisi kuitambua sauti yake na uongozi wake katika maisha yetu. Watu wanaofanya kazi  benki hufundishwa jinsi ya kutambua noti pandia kwa kuichunguza kwa makini sana hadi wanatambua ipi ni bandia na ipi sio bandia. Pia lazima tulijue neno la Mungu ili anaponena nasi na kutuongoza, iwe wazi ni Mungu anafanya hivyo. Mungu hunena nasi ili tuuelewe ukweli. 

  Mungu anaweza nena na mtu kwa njia ya sauti, Lakini Mara Nyingi Mungu hunena nasi kupitia neno lake na wakati mwingine kupitia Roho Mtakatifu kwa akili yetu, hali fulani au mazingira fulani, na kupitia watu wengine pia.