May 15, 2015

Mikono ya kichawi/kishetani - Mchungaji Gwajima

Biblia inasema “mikono ya Mungu si mifupi hata ishindwe kutuokoa” na Yesu kristo alipokuwa msalabani alipigiliwa misumari mikononi mwake.

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Yohana 4:24

Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani. Zaburi 29:11

Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako wa kuume; Na tawi lile ulilolifanya Kuwa imara kwa nafsi yako. Zaburi 80:15

Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako. Zaburi 88:5

Hata Yesu alipaa mbinguni na kukaa mkono wa kuume wa Baba yake. Mungu ingawa ni roho ana mkono na vidole.

Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Luka11:20-22

Yesu alipowaambia wanafunzi wake anatoa pepo kwa kutumia kidole cha Mungu alikuwa ana maanisha anatoa kwa uwezo Roho mtakatifu na ndiye kidole cha Mungu. Shetani naye ana mkono wake na kidole chake. Ndio maana watu wengi wanamwabudu Mungu kwa kuimba Mungu niguse niguse Bwana.

Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. 


Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. 

Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. 

Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana. Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. 


Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. 

Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe. Ayubu 1:8-21

Mtu anayependwa na Mungu ni Yule mkamilifu, mwelekevu, mweye kumcha Mungu, mwenye kuepuka uovu na Mungu hujisifu naye.


Shetani anamwambia Mungu kwamba Ayubu anakucha kwasababu umembariki na kazi zake zimebarikiwa, na mali yake pia imebarikiwa maana Bwana akamwambia gusa hivyo vyote alivyo navyo lakini usinyooshe mkono wako juu yake. Unaweza kuona wachawi ambao ni mawakala wa shetani nao kabla hawajamloga mtu hujaribu kumgusa kwanza.

Kuna watu ambao wana matatizo kwasababu wameguswa na mkono wa kichawi lakini wao hawajui. Mungu alimruhusu shetani anyooshe mkono juu ya vyote alivyo navyo Ayubu lakini asinyooshe mkono juu ya roho yake mwenyewe, lakini Ayubu hakujua kama ni shetani ametia mkono juu yake, Na cha ajabu matukio yakaanza kumpata.

Shetani aliponyoosha mkono wake wakatokea waseba (wezi) wakaiba mifugo na kuondoka nao. Ayubu hakuwepo yeye pekeyake mwenye mifugo bali walikuwepo na wengine wenye mifugo lakini hao hawakuibiwa. 


Cha ajabu alipigwa na wajakazi wake wakamjia na kumwamibia watoto wake wamekufa, ngamia zake zimechukuliwa, na aliposikia hayo alichanganyikiwa na hapa kume tunajiunza shetani anapomgusa mtu kwenye maisha yake kwa mkono wake mtu huyo anaanza kuchanganyikiwa na Ayubu aliamua kurarua nguo zake na kunyoa kichwa chake na kusujudia na kumwomba Mungu akisema Bwana litoa na Bwana ametwaa. 

Lakini hapa Bwana alitoa kweli kwa kumpa mali na vyote alivyokuwa navyo lakini si yeye aliye vitwaa bali ni shetani ndiye aliyevitwaa. 

Imeandikwa tutaweka mikono yetu juu ya wagonjwa nao watapata afya hii inamaanisha Yesu aliweka mkono wake kwa kijana naye akaamka, aliweka mkono wake kwa mgonjwa naye akapona na sisi tunaye mtumikia ametupa mamlaka yakuweka mikono yetu juu ya wagonjwa nao kapata afya.

Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake. Danieli11:16

Ee Bwana, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha hatua zangu. Zaburi140:4
kuna mikono ya watu ambao ni watumishi wa wachawi akikushika unapatwa na mikosi kwamaana wao hawana haki mbele ya Mungu.

Bwana amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake. Zaburi 9:16


Wachawi wanaweza kujua uko sawa au hauko sawa pale wanapokushika mkono. Inawezekana kuna mkono wa kishetani uliwahi kukugusa ama una nguo au viatu unavyo viliguswa na mchawi na kunuiziwa maneno mabaya juu yako ambayo yanakupata bila wewe kujua lazi ikatwe na kurudishwa kule ilipotoka.

Maombi


Mikono ya wachawi waliowahi kugusa mikono yangu nguo zangu, chakula change, mali zangu zote kuanzia sasa kwenye ulimwengu war oho ninafuta alama zao kwa jina la Yesu.


Kila unapoamka unapoomba unatakiwa uombe kwa damu ya Yesu ninaitakasa mikono yangu uso wangu, mwili wangu ninaitakasa kwa damu ya Yesu. Usiwaogope na kwa kwa kuwepa unatakiwa upambane nao kwa jina la Yesu. Kila aliyegusa nguo yako kwenye ulimwengu wa roho leo tunamrudishia vyote alivyoviweka kwa jina la Yesu.Ukiguswa na Mungu ile nguvu inaingia mpaka kwenye mifupa ndani ya mwili. 

Kwa jina la Yesu mikono ya kichawi iliyogusa vitu vyangu mwili wangu au kitu chochote ninavifuta kwa jina la Yesu, alama za kichawi zilizoachwa ndani ya nguo zangu ninazifuta kwa damu ya Yesu, mikono ya kichawi iliyogusa ndoa yangu, familia yangu, kazi yangu ninaamuru kwa jina la Yesu ivunjike kwa jina la Yesu kristo, ninanyoosha mkono wa Mungu kuivunja na kuiteketeza mikono ya kishetani iliyo nyooka juu ya maisha yangu ninaivunja kwa jina la Yesu kristo, imeandikwa 
UFUNUO12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo” kila mchawi aliye nyoosha mkono wake juu ya mwili wangu, nguo zangu, kichwa changu, kanisa langu, nchi yangu, ndoa yangu, nchi yangu ninaipoozesha kwa damu ya mwana kondoo, kwa jina la Yesu kristo.
Kila mkono wa kishetani ulionyooka ili kuleta maangamizo juu yangu ninaupoozesha na kuuvunja kwa jina la Yesu kristo, ninatuma polio kwenye mikono yote ya kichawi iliyojipanga kugusa watoto wangu, biashara yangu, elimu yangu ninaipoozesha kwa damu ya Yesu kristo, ninaivunja kwa jina la Yesu kristo. 

Kila kazi iliyoanzishwa na mikono ya kishetani ninazibatilisha kwa jina la Yesu kristo, ninaamuru kwa mamlaka ya Jina la Yesu kila mkono wa kichawi ulionyooka kunigusa mimi na familia yangu ninaipoozesha kwa damu ya Yesu krito ninaipoozesha kwajina la Yesu, ninaifyeka kwa jina la Yesu kristo.

Mikono inayoleta utasa ninaivunja kwa jina la Yesu ewe mkono ulionyooka kuleta utasa kazini kwangu, utasa kwenye elimu ninakuvunja kwa jina la Yesu kristo, kila mkono wa kichawi uliotumwa kunigusa mimi na vyote nilivyonavyo leo ninakuvunja kwa jina la Yesu kristo, ewe shetani uliyenyoosha mkono wako kuniletea uoga wakati wa usiku na hofu wakati wa mchana leo ninakuvunja kwa jina la Yesu kristo, kila mkono ulionyooka kwa watoto wangu, wazazi wangu, rafiki zangu, na ndugu zangu wote leo ninaondoa uweza wako wa kudhuru na kukuvika polio upooze na ninakufyeka kwa jina la Yesu kristo, ninaukata mkono ulio nyooshwa ili nisiolewe kwa jina la Yesu, ninaukata mkono ulionyooshwa ukagusa nguo zangu, mali yangu au chochote nilicho nacho kwa jina la Yesu, ninaukata mkono ulionyooshwa kugusa ajira yangu kwa jina la Yesu, ninaukata mkono wa wachawi ulionyooshwa kugusa mapato yangu kwa jina ya Yesu, mchawi mwanaume,mtoto,mwanamke, mzee ninaukata mkono wako uliounyoosha kunigusa mimi na mali zangu kwa jina la Yesu kristo.

Amina.