• Isikupite Hii

  May 20, 2015

  SOMO: KUHARIBU MAZAO YA NDOA ZA KISHETANI / KICHAWI.

  Mchungaji Gwajima

  Tulijifunza wiki iliyopita kwamba kuna majini yanaoa watu kwenye ulimwengu wa roho au ndotoni. Ndoto ni bayana watu wote walioota ndoto zilikuwa kweli. Mfano,
  - Yakobo aliota ndota ikawa kweli, 
  -mfalme aliota ndoto ikawa kweli 
  - mamajusi wa mashariki waliota ndoto ikawa kweli.

  Na leo watu wanaota ndoto kwamba umelala na mtu, anakuja na kulala na wewe kitandani, lakini mtu anapoamka anasema ni ndoto tu.
  Siku moja niliota napiga kifaru kilikuwa mlimani nikatuma moto kikalipuka.
  Ndoto ni bayana na ukipuuzia yatakupata uliyoota. Mtu ambaye anaota amelala na mtu anakuwa na matatizo kwenye maisha yake, kama hajaolewa hawezi kuolewa , au ndoa yake inakuwa na matatiozo. kama wewe ulikuwa unaingiliwa kimwili, au unalishwa ndotoni ujue mashetani yanajiimarisha.

  Makuhani wa nchi ndio wanahusika kulisha watu vyakula ndotoni, makuhani ni watu wanaomwakilisha shetani, Yehova awe na makuhani wake na ibilisi naye ana makuhani wake.

  Masheni wanapoona mapepo yamepigwa yamenyongonyea wachawi wanaamua kwenda kumlisha mtu ndotoni ili kumpa joka yule nguvu, sasa mwanakondoo ameshinda lazima shetani na malaika zake waondoke na leo wanateketezwa kwa jina la Yesu.

  Sasa unapoona wanaanza kukulisha ujue kwamba wanataka kurudi, ni sawa na mume ambaye hana nguvu katika nyumba, leo tunaakikisha kwamba lazima aendele e kunyongonyea na chakula chake cha ndotoni ukiletewa ukikatae kwa jina la Yesu,

  Wakati mapenzi ya ndotoni yanaendelea kuna watoto wanazaliwa lakini siyo watu ni mashetani ,yaani wana akili lakini siyo watu,mtu kama huyo haitaji maombi ila anatakiwa kuondolewa. kama mpinga kristo atazaliwa na mtu atakuwa na akili nyingi sana darasani atakuwa na akili kwenye kila somo lakini siyo mtu.

  Sasa kuna mazao ya kishetani mtu alikuwa anaingiliwa lakini hajui yeye, sasa leo tunafanya msako na kung'oa mazao ya kishetani na kumpanda ya mbinguni ,leo kuna msako wa kuteketeza wananchi wa kuzimu na kupanda raia wa mbinguini ,ili mwana wa kuzimu awe wa kuzimu na wa mbinguni awe wa mbinguni, 
  leo ninaanza polepole lakini lazima nimng'oe mtu wa kuzimu, walokole wote tuna asili ya Mungu , tunatembea na asili ya mbinguni

  Mwanzo 6: 1-4,
  Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 
  2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 
  3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 
  4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao 
  Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao.

  Manefili maana yake ni majitu kwenye mstari wa nne , Mungu alikasirika sana baada ya kuona wana wa Mungu wanoana na wana wa wanadamu , akafupisha miaka ya kuishi kutokea miaka mia nane mpaka miaka mia na ishirini, lakini tunaona waliozaliwa baada ya binti za Mungu kuoana na binti za wanadamu.

  Hawa binti za wanadamu ni akina nani na wana wa Mungu ni akina nani?
  Maana ya kwanza ni kwamba Adamu alizaa watoto wawili Kaini na Abel, watoto wa Kaini ndiyo wana wa wanadamu, na Sethi alizaa wana wa Mungu, kwenye maana ya pili ya mbinguni ni hii, kwenye biblia mtu anapoitwa mwana Mungu, maana yake ni roho 
  Yohana 3:6,
  Mungu anazaa roho kwa maana naye ni roho, ni kwa mfano ukizaliwa na nguruwe na wewe ni nguruwe, ukitaka kujua asili ya mtu fuatilia kazaliwa na nani, wakati biblia inaandikwa manefiri walikuwa wametoka duniani, hebu tuangalie ukweli huu, manefiri hao ni malaika, malaika katika utawala wao wanatamani sana kuwa kama wanadamu ndiyo maana wanang’ang’ania kujiungamanisha na wanadamu.

  Hesabu 13:33 
  Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

  Wana wa Israel walikutana na manefiri walipokuwa wanatoka Misri kwenda kanaani, manefili walikuwa duniani nyakati zile, hawa manefili duniani ni majitu yenye nguvu, Kumbukumbu 3:11, kwenye Zaburi 136:17,
  Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

  Daudi aliimba akamtaja hata Sioni na Ogu wafalme wa bashani na Amoni , kumbe Ogu alisalia katika wana wa manefili ,ndiyo maana Daudi anaimba kwa kuliua jitu hilo, lenye urefu wenye mita tisa , na Goliath ni mmojawapo wa mabaki ya majitu yale, niwaangalie kidogo hao wanefili 
  Kumbukumbu 9:2, 
  watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki?

  hapa wana wa Israel waliambiwa mnakwenda kwenye nchi ya kanaani ambapo kuna majitu ambayo yanatajwa tajwa, kuna malaika waliotupwa waliamua kuvaa miili na kuungana na wanadamu kwa kuoa, Wale ambao walikuwa wanauana kipindi kile mbele za mungu hawakuwa watu, ndani yalikuwa majoka yaliyovaa miili.

  Ndiyo maana kuna mahali Mungu anawaambia watu wa fyeke fyeke na kila mahali panapotoa maji pafukie Kwa sababu mbele zake walikuwa siyo watu. Kwa hiyo najaribu kukuonyesha kwamba manefiri walikuwepo, Mungu akaona bora hafupishe miaka ili majitu yasiendelee kuishi miaka mingi , hiyo ndiyo theologia ya kweli.

  Nikaona research ya watoto wanaozaliwa muhimbili asilmia 75% ya watoto wanaozaliwa siyo baba zao wa uhakika, nikafikiri kwamba wanawake siyo waaminifu , kumbe siyo ni yale mabwana ya ndotoni, ndiyo maana kunaongezeka watu wa ajabu, yaani nyakati tulizofika huwezi kuyazuia mabaduiliko , ukikataa kubadilika, mabadiliko yatakubadilisha wewe.

  Kwa jina la Yesu mtu yeyote asiye mwanadamu namwangamiza leo kwa jian la Yesu.

  Sasa unakuta mtu ameolewa na jini na kuzaa watoto ambayo ni majitu na hawa ndiyo wanaosumbua sana duniani, katika Jina la Yesu, leo nakufunga mkuu wa anga na mkuu wa bahri na mkuu wa vichujuu na wachawi wote wa Tanzania na majoka wote waliovaa miili nawafunga wote kwa jina la Yesu.

  Leo tutakwenda kufyeka wanadamu wote ambao ni mazao ya kishetani. Mungu anawabariki watu ikiwa uchumi wanchi ni mzuri, watu wanapokuwa wanapewa mishara mizuri, hospital nzuri zipo na elimu mzuri lakini kana utawala una watu wa ajabu ajabu yaani majitu.

  Nehemia 13: 23-26,

  Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu; 
  24 na watoto wao wakanena nusu kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kunena kwa Kiyahudi, bali kwa lugha ya watu hao mojawapo. 
  25 Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. 
  26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.

  Kwa hiyo inawezekana jini anapoanza kumfuata mtu na kufanya mapenzi naye, mtoto anaweza kuzaliwa. Nje ni mtu lakini kwa ndani siyo mtu ni shetani. Kuna mtu yuko hapa ni zao la ndoa za rohoni ndiyo maana unajiona ni wa ajabu ajabu, kuna wengine usiku unaota amezaa watoto siyo kwamba umeota ni kweli umezaa watoto wa kijini, na wale wanaporudi ujijini wanakurudi na kukuletea wewe matatizo.
  Kwa jina la Yesu leo nafanya vita na kila mtu wa uzao wa kishetani namung’oa kwa jina la Yesu. Nakataa kwa jina la Yesu kama kuna mtu yeyote aliyezaliwa rohoni kutoka tumboni kwangu leo namteketeza kwa jina la Yesu.

  Inawezekana hata wewe ulizaliwa kwa namna hiyo ndiyo maana unapolala unaanza kujiona siyo wa kawaida , leo Mungu atashuka kwa moto na kumchunguza kila mtu na asiye mtu lazima leo ateketee kwa jina la Yesu. Chochote kilichozaliwa cha kichawi leo nakiteketeza kwa jina la Yesu, kuna mtu amezaliwa kwa dawa na huyo anakuwa na matatizo kwa maana mashetani wanamfuata wakidai kuwa ni mali yao, leo ninakana kwa jina la Yesu asili ya kishetani ya ukoo wetu, akili ya kijini, matoto ya kijini naamuru chukueni matoto yenu kwa jina la Yesu, sina uhusiano nayo maana mimi ni mwanadamu na nyie ni mashetani.

  Dalili za mwanamke mwenye mume wa kiroho

  1. Hapendi kabisa kuwa karibu na wanaume, kwa kuwa tayari ana mume wa kiroho
  2. Akichumbiwa lazima aharibu uchumba mwenyewe , lazima atabadilisha mawazo na kusema simtaki mwaume huyo tena, yule jini ndiye anamletea mawazo ya kukataa mwenyewe
  3. Kama akikaribia kuolewa lazima atakataa lakini baadaye umri ukienda anajisikia vibaya 
  4. Kama aking’anga’ana na kuolewa hawezi kuifurahia ndoa yake kabisa ataona ndoa kama ni mateso, vile vile hawezi kumpenda mume wake kabisa , mumewe akiwa mbali anamumiss akija anajisikia kumchukia kabisa,
  5. Kama ameolewa hawezi kupata mtoto kwa maana Yule mume anaona wivu kuona mkwewe anazaa na mume mwingine, Hata kama akifanya biashara hawezi kufanikiwa kabisa kwa maana jini yule anammiliki.

  Mwanamke aliyeolewa na jini huwa anawekewa alama zifuatazo ili aendelea kumilikiwa na huyo jini
  1. Na kila mwanamke anayeolewa anakuwa na cheti cha ndoa, huwezi kukiona rohoni lazima kinakuwepo kama hati ya kumilikiwa.
  2. Alama nyingine ni alama ya ndoa ambayo ni pete ya kiroho, mtu anaweza kuokota pete au kuota anafunga ndoa na kuvalishwa pete 
  3. Alama kama chapa au chata , mtu anaweza kuwekewa alama kama chata /chapa rohoni na hiyo alama inampa mamlaka jini kummiliki mtu.

  Matendo 16:13
  Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.

  Mungu huwa anaweka maelekezo ndani ya moyo wa mtu, sasa moyo wa mtu unaweza kuibiwa na kupewa moyo wenye maelekezo tofauti, maana yake umewekewa alama moyoni ya kushindwa, ndiyo maana ukisema huyo hawezi kuwa kiongozi maana yake ni maelekezo hasi, kwa jina la Yesu leo nakataa moyo wa kushindwa , kuanzia leo nitakuwa mbunge , nitasafiri nje ya nchi, nitaolewa na kuwa na ndoa njema,
  Amen.

  Source: Gospel Kitaa