June 2, 2015

SOMO: MIMI SIO KAMA WALE - MCHUNGAJI GWAJIMA

Mchungaji Josephat Gwajima, mwanzilishi na kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima.


UTANGULIZI:

[ Zaburi 118]
(Luka 4: 14-) Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. 

15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. 
16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 

17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,


SOMO

Yesu alizaliwa akiwa mtu wa kawaida na siku moja alienda katika mto Yordani akabatizwa na kisha akaenda jangwani kwa muda wa siku arobaini na alipotoka huko alienda Galilaya kwenye masinagogi huko akihubiri na kurudi Nazareti katika sinagogi lililojengwa ukingoni na alipofika alipewa kitabu cha Isaya akisema roho wa bwana yu juu yangu amekwisha kuyatimiza mambo haya, na alipokuwa anafundisha walikasirika kwa maneno yale na wakataka wakamtupe wanampeleka kwenye shimo la ukingo na wakati sio desturi yao ya kumtupa mtu kwenye ukingo (wayahudi wao hupiga kwa mawe) na hawakujua kuwa yeye sio kama wao na hii inaonyesha ni kawaida yao kuwatupa watu kwenye ukingo lakini wakasahau Yesu sio kama wao na aliwaponyoka na kupita katikati yao.

Inashangaza sana kwamba Yesu alianza kazi yake kwenye sinagogi hili lililo jengwa ukingoni na inaonyesha ilikuwa ni desturi yao kuwatupa lakini Yesu hakuwa kama wao waliotupwa awali na wewe unatakiwa useme “MIMI SIO KAMA WAO”. Walipowaona wale waliowapa presha wamepatwa presha wakafikiri na mtu wa ‘ufufuo na uzima(YESU)’ atapatwa wakadhani ni kama wale lakini sisi sio kama wale waganga wa kienyeji, wachawi, wasengenyaji, wazushi na tumepewa uwezo wa kuanza na kumaliza mauti yetu sio ya kuangukia kwenye ukingo, mauti yetu ni ya msalaba. 

Waje waganga, wanasiasa na wataabishaji wote na wote wawezavyo ila mjue mimi sio kama wale.
Yesu alisema maneno ya kawaida tu lakini yaliwaudhi hawa mabwana waliokuwa wanasikiliza wakata kumtupa ukingoni maneno yenyewe yalikuwa; 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” maneno haya yaliwapelekea kukasirika hadi kuchukua uamuzi wa kutaka kumtupa kwenye ukingo ndio maana waka kasirika. Wakiulizana huyu si mototo wa seremala huyu?! Si amezaliwa tunamwona iweje leo aseme andiko hilo limetimia kwake?! Kwa wayahudi ukisema Roho wa Bwana yu juu yangu ni vita hiyo umetangaza kwa maana Samsoni alisema roho wa Bwana yu juu yangu akaushika mlango akaung’oa’ ndio maana wale mabwana wakajua huyu Bwana sio wa kawaida anataka apigane ndio maana wakambeba mzobemzobe kwasababu alisema Roho wa Bwana yu juu Yangu na sisi Roho wa Bwana Yu juu yetu katika kazi tunayo ifanya.

Kwa kawaida Israeli ni wanne tu wanaotakiwa watiwe mafuta
1. Mfalme anapotaka kutawaza watu wake 
2. ni kuhani anatiwa mafuta ili asimame kati ya Mungu na wanadamu 
3. Mwingine ni nabii ili awe kinywa cha Mungu 
4. Vyombo vya hekalu ili vitengwe kwa ajili ya kazi ya Bwana

Ndio maana mfalme wa Babeli alienda akaviteka akavichukua vile vyombo vya hekalu akavichukua lakini Nebkadneza akavitunza na alimjua Mungu wa Israeli na baada ya miaka mingi mwanae asiye mjua Mungu wa wayahudi akawa mtawala(mfalme) na siku moja akiwa na rafiki zake wanakunywa pombe akaagiza vile vyombo ili wavinywee pombe na akavigawa wakati Baba yake alivitunza na walipoanza kunywa waliona mkono unaanza kuandika kwenye ukuta kwasababu wamechezea vyombo vilivyo tiwa mafuta na mkono ule uliandika menemene, tekene na peresi na maneno na hakukuwa na lugha iliyoyafahamu maneno yale na mfalme alipoona yale maandishi alisema hawezi kulala hadi afahamu maana yake ni nini na akamwita Danieli amsaidie, Danieli akaviangalia vilee vyombo akaangalia na maandishi ukutani akamwambia mfalme umeumia kuna jambo kubwa limetokea kwenye nchi yako ee mfalme na akaanza kumwambia maana ya mene ya kwanza ni ufalme wako umepimwa umeonekana umepungua na tekeli ni kuna mwenzako amepewa ufalme wako na Biblia inasema usiku uleule mfalme akavamiwa akauwawa na inamaanisha kwamba wale waliokutesa na wataabishaji wako wote wamepimwa wale na hukumu yao ipo watatoweka kwa jina la Yesu.

Jambo jingine alilosimema Yesu ambalo liliwaudhi ni; Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 
Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 


Bila shaka kulikuwa kuna vizee vimewafunga watu ndio maana wakakasirika na kumtoa nje. Na wengi hata sasa wamewafunga watu na wanapo sikia unatangaza unataka kuwafungulia wanakasirika Isaya14:17 Asiye wafungulia wafungwa waende zao’ (zaburi68:6) (yeremia32:44) Mungu anao mpango wa kuwarudisha wafungwa ndio maana Yesu alisema nalikuwa kifungoni hamkuja kuniona na watamuuliza ni lini ulikuwa kifungoni na yeeye atasema mlivyowatendea wale mlinitendea mimi.

Na inawezekana wewe umekwenda msikitini bismilai au kanisani salamu maria lakini hakuna linalosaidia ila anahitajika mtu kama raisi mwenye mamlaka ya kuwaachia wafungwa kuwa na mamlaka ya kufunguliwa kwako na inawezekana umelogwa au hujaokoka wewe ni mfungwa na Biblia inasema “yeye atendaye dhambi ni mfungwa wa dhambi” na utaendelea kupatwa na matatizo na ili ufunguliwe lazima liwepo tangazo nakutangazia siku ya leo ufunguliwe kwa jina la Yesu na kumbuka ulikotoka taabu zote ulizopitia na umesahau unatakiwa ukumbuke ulikotoka na umtukuze Bwana umwambie sijafanikiwa sana lakini leo niko Ufufuo na uzima na ole wake atakaye fanikiwa amsahau Bwana. Ndio maana Paulo aliwaambia enyi wagalatia msio na akili ni nani aliye waloga maana mlianzia Rohoni sasa hivi mnaishia mwilini?

(Yeremia 33:26 49:39) (ezekieeli 16:13) (hosea6:11) (zefania 2:7) Yesu akasema Bwana amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao (matendo27:42) kwa neno hilo walimtoa ndani ya sinagogi wakataka kumtupa.

Lakini sisi tumetumwa kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na Yesu aliwatuma wanafunzi wakamfungue mwanapunda na akawaambia mwenye punda atawauliza nanyi mwambie Bwana anahaja nae hapa tuna jifunza kuwa wale waliofunga wana kawaida ya kuuliza na jambo ametokaje, anaendeeleaje ameolewaje, amesafirije lakini sisi tunawaambia kuwa ni Bwana?

Lingine lililowaudhi ni , “Na vipofu kupata kuona tena”, Kuwaacha huru waliosetwa, kumbe kuna walio kuwa wanaona lakini wamefanywa vipofu lakini wanatakiwa kuona tena, ile ndoa yako iliyofungwa leo uione tena kwa mamlaka ya jina la Yesu watu wanatakiwa waone tena na hakuna atakaye zuia lazima waone tena. Nakataa kutumbukia shimoni kama wale, nakataa kulogwa kama wale kwa jina la Yesu.

Na jambo lingine lililowaudhi ni amekuja kuwakomboa waliosetwa(banwa) kuwaweka huru walioteswa. Pengine unasema familia yetu hakuna aliyesoma shule mimi nitasomaje! unatakiwa useme mimi sio kama wale.

Pia jambo jingine lilikuwa amekuja kutangaza mwaka Bwana kwa nia ya kuwaachilia wafungwa na wote ambao wamefungwa kwa muda mrefu na waliposikia hivyo walitaka afe isivyotakiwa kwa kumsukumia shimoni ukingoni lakini alipita katikati yao na biblia inasema hakuna mfupa wake hata mmoja uliovunjika. Sema nakataa mimi sio kama wale kwa jina la Yesu.


MAOMBI:

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Kwa jina la Yesu kila aliye andaa shimo, shimo la mauti shimo la balaa ataingia yeye mwenyewe kwa jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu ninafanya vita najitakasa kwa damu ya yesu wale walionisukuma kwenye ukingo waliouandaa nawatumbukiza wao kwa jina la Yesu. Ninakataa kutumbuikia kwenye shimo waliloliandaa kwa damu ya mwanakondoo ninawatumbukiza wao kwa jina la Yesu, mimi sio kama wale mliowatumbukiza, nakataa kutumbukia kwa jina la yesu nawatumbukiza wao wenyewe mimi sio kama wale ulio wanywesha sumu, ulio waloga, uliowatumbukiza shimoni, uliowarudisha nyuma nakataa kwa jina la Yesu, nawatumbukiza nyinyi kwenye mashimo mlioniandalia kwa damu ya mwana kondoo mimi sio wa kukatishwa tama kama wale mimi sio wakuburuzwa kama wale nakataa kwa jina la Yesu, “nena kwa lugha kama unanena ...........kataa mimi sio kama wale kwa jina Jina la Yesu.

Source: GospelKitaa