July 21, 2015

EXCLUSIVE: RUNGU LA YESU KUACHIA WIMBO MPYA SPECIAL KWA AJILI YA WIFEY (MKE) WAKE.Rungu La Yesu Akizungumza na blog hii Ya Tim Heaven Alisema kwamba jumamosi hii ya Tarehe 25 mwezi huu wa 7 anatarajia kuachia wimbo mpya "ZAWADI" special kwa ajili ya mke wake mtarajiwa "Nuru Samson". Binafsi nilipata nafasi kidogo ya kusikiliza wimbo huo japo ilikuwa ni demo lakini niliinua mikono juu, maana ni bonge bomba la ngoma yani ni wimbo mkali sana.

Wimbo umefanyika GOOD NATION Chini ya Masebo

Najua wengi tuna-maswali mengi vichwani, kwamba ni lini na wapi harusi hii itafungwa, Harusi hii itafungwa jumamosi hiyo hiyo ya tarehe 25 mwezi wa 7, Ukisikia kwa Yesu ni double sasa ndo hii hapa. 
Hakikisha Umelike page ya Rungu La Yesu Facebook kwa taarifa zaidi.