August 21, 2015

ASKOFU MKUU (KKKT) AWATADHARISHA WAGOMBEA KUHUSU SWALA ZIMA LA UCHAGUZI.


Askofu Mkuu wa kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania (KKKT). Frederick Shoo amewatadharisha wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini kutambua kua kuna maisha baada ya uchaguzi mkuu.

Alisema kwamba ni vyema wakafanya kampeni zao kwa amani ili kuiepusha nchi kuingia kwenye machafuko. 

Pia, amevitahadharisha vyombo vya usalama kuhakikisha vinasimamia kiapo walichoapa pindi walipoanza kazi ya kutetea haki na kulinda amani ya chi bila kupendelea upande wowote.

Source: Mwananchi.