August 19, 2015

NEWS: BINTI WA MIAKA 19 ACHARAZWA BAKORA 20 KWA KOSA LA KUVAA SURUALI MTAANI

Mfano wa vazi la suruali likiwa limevaliwa na mwanadada. picha hii haihusiani na habari. 

Binti mwenye umri wa miaka 19 mbaye ni mkristo huko nchini Sudan alijikuta hatiani kwa kutandikwa bakora 20 kwa kosa la kuvaa suruali mtaani wakati akitoka kanisani kwenye ibada. Binti huyo aliyefahamika kwa jina la Fardos al-Toum ni miongoni mwa wanawake wakristo 12 waliokamatwa June 25 mwaka huu kwa kosa la kuvaa suruali na sketi wakitokea katika kanisa la Baptist jijini Khartoum. 

Fardos alikuwa wa kwanza miongoni mwa wasichana wadogo kuchapwa bakora katika utekelezaji sheria ya kutovaa mavazi hayo ambayo si ya heshima kwa mujibu wa dini ya kiislamu nchini humo sambamba na kutakiwa kulipa faini ya pound 500 za Kisudan ambazo hata hivyo zililipwa na wanaharakati wa haki za binadamu. 

Aidha katika taarifa nyingine kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Marekani CNN zinasema mwanasheria wa binti huyo naye pia ametakiwa kuchapwa bakora 20.

Taarifa zinasema mara baada ya kukamatwa kwa wanawake hao, wasichana wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 17 na 23 walipelekwa kituo cha polisi ambako wawili kati yao waliachiwa huru huku wengine 10 waliamriwa kuvua nguo zao na kwamba walishikiliwa kituoni hapo kwa masaa 24 na kuandikiwa makosa ya kuvaa mavazi yasiyoruhusiwa.

Mwanasheria anayewatete wanawake hao Muhamad Mustafa amefungua kesi kupinga hukumu ya Fardos kwakuwa wasichana wengine waliokuwa wamevaa kama yeye hawakuchapwa wala kulipishwa faini kama ilivyokuwa kwake. Huku wanawake wengine wanne walitakiwa kulipa faini, wengine wanne walifutiwa makosa huku mmoja wao akisubiri mashtaka yake. Wasichana hao walikumbwa na kosa la kuvunja sheria ya Sudan kifungu namba 152 ya mwaka 1991 kosa ambalo adhabu yake hufikia kuchapwa bakora 40. Wakristo na waumini wa dini nyingine sio ya kiislamu wamejikuta kwenye matatizo ya kuvunja sheria hiyo inayosimamiwa na mahakama ya kadhi nchini Sudan. Umeandika mtandao wa Christian Post.

Respect kwa Gospelkitaa.