August 21, 2015

MAAJABU: BIBI AJIFUNGUA SALAMA WATOTO WANNE KWA PAMOJA.


Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 ameweka rekodi ya kuwa mama mzee zaidi duniani baada ya kujifungua watoto wanne kwa pamoja.

Uzazi huo umeonekana kuwashangaza madaktari katika hospital ya Berlin Charite kutokana na umri mkubwa na mwanamke huyo aliyefahamika kama annegret  Raunigk.

Kwa mujibu wa madaktari, watoto hao ambao wte walizaliwa kwa njia ya upasuo zinaonekaaji, afya zao zinaonekana kuimarika siku hadi siku, hali inayoashiria kuwa watakuwa salama.

"Ni mara chache sana kwa mwanamke  wa umri huu kubeba ujauzito na kujifungua salama, tena kwa mimba ya watoto wa nne. Lakini kwa annegret hali imeonekana kuwa tofauti, anaendelea vizuri yeye na watoto wake," Alisema Profesa Christoph Buher.