Featured Posts

August 24, 2015

NEWS: ZAIDI YA WATU 50,000 WAJIANDIKISHA MARA MBILI BVR.


Tume ya Taifa ya Uchungizi (NEC) Imebaini watu 52, 062 wamejiandikisha zaidi ya mara moja wakati wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga Kura.

Mkurugenzi wa Nec, Kailima Kombwey alisema jana kuwa tayari watu 12 wamehukumiwa kifungo cha kati ya mwaka mmoja mpaka miwili.

"Watu wengine tunatarajia kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria," alisema Kombwey na kuongeza:

"Uhakiki wa taarifa Dar es salaam unaendelea na mpaka kesho (leo) kila kituo kitakuwa kimepata daftari."

Wakati huohuo: Kamati ya kuangalia Mwenendo wa Uchaguzi Tanzania (Temco) imesema bado kuna haja ya serikali kuwashirikisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu.

Mratibu wa Temco, DK Benson Banna alisema hayo alipotoa ripoti ya awali ya uchunguzi katika uandikishaji wananchi katika Daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa (BVR)

Source: Mwananchi.