August 2, 2015

NEWS: ISIS KUTOA ZAWADI YA KICHWA CHA BINADAMU KWENYE HARUSI YA JAJI WAO.


Baadhi ya wanajeshi wa kikundi cha ISIS

Hatma ya maisha ya mtu nchini Syria iko mikononi mwa kundi la kiislamu la IS, tofauti na tamko la haki za binadamu la umoja wa mataifa, kitu chochote utakachofanya ambacho kitaelekea kutowafurahisha, basi hatma ya maisha yako itakuwa mikononi mwao, halikadhalika wakihitaji kufanya jambon la kuwafurahisha, hata kama ni kuua mtu kikatili, basi watatekeleza hilo ili wapate 'furaha'. 

Hali hiyo ndiyo inayoelekea kumtokea mwanamama mmoja ambaye amekuwa jaji kwa muda mrefu akifanya kazi chini ya utawala huo dhalimu, ambapo hivi karibuni jaji mwingine alifiwa na mume wake, basi katika harakati za kuolewa tena, mwanamama huyo akaomba zawadi ya kichwa cha mtu.. 

Katika kutafakari, na baada ya kutambua kwamba mwanamama huyo hawezi kuzawadiwa kichwa cha mwanaume, ikaamriwa na kiongozi wa IS, Bwana Abu Bakr al-Baghdadi, kwamba jaji mwingine mwanamke achinjwe ili mjane huyo, Roaa Um Khotaba al-Tunisi  aitimize ndoto yake. Hayo yote yakamuangukia mwanamama mwenzake, Um Abdullah kutokana na kuhisiwa kwamba kazi yake kubwa ni kuwapeleleza IS na kisha kupeleka taarifa zao kwa wabaya wao. 

Picha ya katuni ikionesha wanajeshi wa isis wakiwafundisha watoto namna ya kuchinja

Akieleza kwa hofu, mmoja wa wafanyakazi waliotoroka kuhofia usalama wao (jina limehifadhiwa), ameieleza Daily Mail ya Uingereza kwamba hali za namna hiyo ni za kawaida sana kwenye utawala wa IS, na kwamba anajuta kuungana nao, kwani hadaa walizopata ndio zilipelekea yeye na familia yake waamini kwamba hiyo ndio dini ya kweli ya kiislamu, lakini mwisho wa siku kutokana na yaliyokuwa yanajiri, akaamua kutoroka, na hadi hivi sasa akilazimika kubadili makazi kila mara kuhofia kupatikana. 


Matukio ya kuchinja kwa kundi la IS yamekuwa ya kawaida, ambapo mwanzoni mwa mwezi Juni mwanajeshi wa Libya alichinjwa mbele ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6 hadi 8, nchini Libya, ikielezwa kwamba ni kwa madhumuni ya elimu tu. "educational purposes". Na hali hiyo ndiyo ambayo wakristo hukutana nayo, ikiwemo waamini wa dini nyingine tofauti na kiislamu, na hata wale waislamu wasio na itikadi kali, pia hufananishwa na wakristo na kuteswa kwa pamoja.

Daily Mail | Russia Today | Gospel Kitaa.