Featured Posts

August 11, 2015

NEWS: KANISA HILLSONG LAWEKA WAZI MSIMAMO WAKE JUU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA .

Mchungaji Brian Houston

Mchungaji kiongozi wa kanisa maarufu duniani la Hillsong Brian Houston wa Australia ameweka wazi msimamo wa kanisa hilo dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kufuatia ripoti iliyokuwa imesambaa katika mitandao kuhusu kati ya waongozaji uimbaji wawili wa kiume wa kanisa hilo jijini New York nchini Marekani  kutangaza hadharani kwamba wanauhusiano wa kimapenzi.

Katika ujumbe wake mchungaji Houston aliamua kuweka wazi kuhusiana na taarifa hiyo kwamba kanisa hilo limeruhusu wanaume hao walioweka wazi uhusiano wao kuimbisha kwaya kanisani hapo. Mchungaji Houston amenukuliwa kupitia blog ya kanisa hilo kwamba msimamo wa kanisa hilo katika suala la mapenzi na ndoa za jinsia moja haujabadirika sawasawa na maandiko yasemavyo. Alisema, kama alivyowahi kuzungumza awali akisema anaamini maandiko ya mtume Paulo yako wazi kuhusu jambo hilo. 

"Miezi michache iliyopita wakati mmoja wa waongozaji wetu wa kwaya alipotoa tangazo kwa jamii ambalo hatukulitegemea kwamba amevalishwa pete ya uchumba na mmoja wa waimbaji ambaye huimba kanisani hapo, lilikuwa jambo la kustua na kushangaza kwetu pia. Katika uelewa wangu ni kwamba hawajawahi kupewa ama kuwemo kwenye uongozi wa kanisa hilo tangu walipotangaza uhusiano wao. Lakini bado tunawapenda na tunajua ni watu kama sisi, tupo kwenye safari moja, na jukumu letu kama kanisa ni kuwasaidia katika safari hii kwa upendo na rehema". alisema mchungaji
Houston.

Katika blog ya kanisa hilo yenye kichwa "Je ninawapenda mashoga? 'Do I love gay people?' mchungaji Houston amesema, Kanisa la Hillsong linawakaribisha watu wa aina zote isipokuwa haikubaliani na aina zote za kimaisha ama kimienendo, ikiwa pamoja na kuwapa nafasi za uongozi wa kanisa watu wenye mapenzi ya jinsia moja iwe kwa kazi ya kulipwa ama ya kujitolea. "Ninajua ujumbe huu utawavunja watu nguvu katika pande zote za jambo hili ambalo pia ni gumzo kwa makanisa yote duniani" aliandika mchungaji Houston.
                          

                                   Mchungaji Carl Lentz

Hata hivyo pamoja na mchungaji Houston kusema inakaribisha watu wa aina zote lakini sivyo kwa watu wanaopanga kuleta fujo ama migongano, watu wanaopenda ugomvi pamoja na wenye tabia za ubakaji na kulaghai watoto wadogo kwa mambo ya ngono" alimalizia mchungaji Houston. Kanisa la Hillsong New York linasimamiwa na mchungaji Carl Lentz aliyetokea kupendwa sana na waumini wa kanisa hilo duniani ikiwemo London kutokana na namna ya ufundishaji wake huku pia mtoto wa kwanza wa mchungaji huyo ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji maarufu wa kanisa hilo Joel Houston anashiriki katika kanisa la Hillsong New York.

Source: GospelKitaa.