• Isikupite Hii

  August 2, 2015

  SOMO: MFALME ALIYEPOTEZA UFALME - ASKOFU GWAJIMA.


  Biblia ni kitabu kinachohusu Ufalme, Mfalme na familia ya kifalme, ni kitabu cha serikali ya Kifalme, ni kitabu kinachohusu katiba ya Ufalme, ni kitabu kinacho husu uchumi wa Ufalme, ni kitabu kinacho husu funguo za Ufalme, ni kitabu cha agano/makubaliano, ni mkataba wa Ufalme, ni kitabu cha sheria ya Ufalme na mila ya Ufalme.


  Yesu alienda kubatizwa katika mto Yordani kabla ajaenda kuomba jangwani kwa muda siku arobaini na alipotoka huko alikuwa amejaa Roho wa Mungu. Maneno yake ya kwanza yalikuwa ni tubuni maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia/umeshafika. Alimaanisha watu wabadilishe namna ya kufikiria kwamba wanatakiwa waishi kwa kuvumilia ili wakaurithi Ufalme wa Mungu na kustarehe mbinguni kitu ambacho sio kweli bali hayo ni mapokeo ya kidini ambayo hayamo kwenye Biblia. 

  Yesu alikuwa anamaanisha watu wabadilike namna ya kufikiria kwasababu Ufalme wa mbinguni umeshafika duniani, na hata alipofufuka aliendelea kufundisha habari ya Ufalme wa mbinguni hapa duniani. Yesu hakufundisha kuhusu damu ya mwanakondoo kwasababu hiyo ilikuwa ni misuli ya kujengea Ufalme wa mbinguni hapa duniani.

  “hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu. 6 Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” Matendo ya mitume1:2-3, 6

  Wanafunzi wa Yesu walianza kumwelewa Yesu kuhusu Ufalme wakati alipofufuka. Paulo naye alifundisha kuhusu habari za Ufalme wa mbinguni.
  “Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.” Matendo ya mitume 28:30 – 31

  Lengo lilomtoa Yesu mbinguni kuja hapa duniani lilikuwa sio kuja kuzaliwa kwenye holi la ng’ombe au kuteswa kwa misumari au kuvishwa taji la miiba kichwani au kuchomwa kwa mkuki ubavuni bali lengo la Yesu kupatwa na yote hayo lilikuwa ni kuujenga Ufalme wa mbinguni hapa duniani na kutununua kwa damu yake ili tumiliki hapa duniani tukiwa kama wana wa Ufale sababu tulikuwa tumeupoteza ufalme huo. Yesu alikuwa anahangaika sana kuuelezea ufalme wa mbinguni jinsi ulivyo kwa mifano mingi sana ili aeleweke na watu.

  “Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini? Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake. Akasema mara ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachacha wote pia.” Luka 13:18, 20

  Yesu alitoa mfano wa Ufalme wa mbinguni ni kama punje ya haradani kwamba ukiingia mahali hauwezi kuonekana lakini baada ya muda unakuwa mkubwa sana na kuenea,Yesu anajaribu kuonyesha kwamba ufalme wa Mungu ni kama chachu ambayo ikiingia mahali inageuza eneo lote, anaonyesha kwamba Ufalme wa Mungu ni kama hazina iliyojificha mahali na ukiiona unaacha vyote ulivyo navyo na kuifuata sababu vyote vinapatikana humo ndani yake, anaonyesha Ufalme wa mbinguni ni kama lulu iliyomahali na mfanya biashara ameiona na akaamua kuuza lulu zake zote na kuifuata lulu hiyo kubwa ya thamani aliyoiona.

  Yesu alivyoona watu wanawaamini na kuongelea habari za kina Musa na Manabii kina Eliya ndipo akaamua kuwaambia kwamba.
  “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati.” Luka 16:16 – 17

  Yesu alimaanisha torati na manabii mwisho wake ni Yohana ndiomaana Yohana alikuwa anawaambia watu “tubuni kwamaana Ufalme wa Mungu umekaribia”.

  Yesu alipoenda mlimani aliongea na Musa na Eliya ambao waliwakilisha manabii na mitume wote, vitabu vyote vya mwanzo vilikuwa vinamwongelea Yesu ajaye. Wanafunzi wa Yesu walipoyaona hayo yakitokea Mungu Baba wa mbinguni aliongea nao akawambia wamsikilize Yesu peke. Maana yake Yesu amekuja kuleta Ufalme wa Mungu kwetu sisi wafalme tulioupoteza kupitia kwa Adamu na Hawa.

  Neno wakristo lilitokea kwenye Biblia lakini halikuwa wazo la Yesu bali wazo la Yesu lilikuwa ni kuleta Ufalme hapa duniani. Yesu hakuhubiri kuhusu mafanikio kwasababu anajua watu wakiingia ndani ya Ufalme watapata vitu vyote bila gharama yeyote.

  “Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa.” Luka 4:43 
  Yesu aliona hawamwelewi akaamua kuwaweka wazi 

  “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.” Luka 12:32 

  Kwenye ufalme wa Yesu hakuna mjadala kwasababu ya sheria zake, watu wote wakishika sheria ya ufalme utakatifu unatawala kwenye eneo hilo, mbinguni sheria ya Ufalme inashikwa kikamilifu ndiomaana utakatifu umetawala. Mungu wa rohoni ameleta Sheria kwa wa rohoni mwenye mwili ili auonyeshe Ufalme wake hapa duniani, anajua kwamba yule wa rohoni anaweza kuutenda ufalme wa mbinguni akiwa ndani ya Ufalme wake. Mungu ambaye ni Roho ameamua kumpa wa rohoni mwenzake ili Ufalme wa mbinguni utendeke hapa duniani ili watu waone sheria ya Ufalme inatenda kazi hapa duniani. Watu wamejaza mambo mengi kwenye nafsi zao badala ya sheria ya mbinguni ndiomaana unakuta mtu anaomba sana na kufunga lakini hajitambui yeye ni nani sababu hajarudisha Ufalme wake uliopotea na kuumiliki akiwa ndani ya Ufalme.
  Mathayo 25:34

  Kabla ya kuubwa kwa ulimwengu Ufalme umewekwa tayari hapa duniani, Mungu kabla hajaumba chochote alikuwa yeye mwengewe kwenye ufalme wake. Wakati ule alipata wazo anataka kutengeneza Ufalme. Aliamua aweke ufalme ili awaonyeshe watu jinsi ya kumiliki na kutawala kama yeye anavyotawala.

  Marko 1:24-25

  Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwamba Yeyote watakayoomba yatakuwa vilevile. Ufalme wa mbinguni ni nchi ya mbiguni ina mfalme ndani yake. Ufalme wa mbinguni ni nchi ya Ufalme yenye lugha ya kifalme, kwa kadiri mila ya ufalme inavyoenea mila za giza zinaanza kufutika zenyewe . 

  Yesu alipokuja hapa duniani hakusisitiza kuhudu kuzaliwa mara ya pili bali aliongea na mtu habari za Ufalme na kumpa sheria ya Ufalme na kuingia ndani ya Ufalme wa Mbinguni kwa kuzaliwa ndani ya Ufalme.
  Yesu ni mzaliwa wa kwanza kwenye Ufalme na ni kaka Yetu mkubwa maana yake sisi tunafanana nayeye ambaye ni mzaliwa wa kwanza kwenye nchi ya Ufalme na sisi ni wazaliwa wa pili.

  Unapoendelea kujitambulisha mkristo falme za giza zinajua hilo jina tumejipa sisi wenyewe na zinajua mbinguni asili yake ni uwana wa Ufalme na ukristo hauna nguvu yeyote. Utambulisho wako ndio utakao kuwezesha kupenya kwenye sehemu fulanifulani kwenye maisha yako. Ukijiita mkristo hauwezi kufanikiwa kwenye baadhi ya mambo lakini ukijitambulisha kama raia wa mbinguni mapepo hayawezi kukugusa au kuingilia maisha yako kwasababu upo ndani ya ufalme wa mbinguni.
  Katiba za duniani zote zinaanza hivi “sisi wananchi” lakini katiba ya Ufalme wa mbinguni inaanza “hapo mwanzo kulikuwa na neno”. Katiba za duniani zinafanya matakwa ya wananchi vile wanavyotaka lakini katiba ya mbinguni inataka sheria za Mungu wanadamu wazifuate wakiwa ndani ya Ufalme hapa duniani.

  Ufalme unakawaida ya kumeza lakini haumezwi na Ufalme huu utaimeza Tanzania na dunia yote.

  Mwanzo 1:26

  Lengo la Mungu lilikuwa ni kujenga ufalme duniani na amfanye mtu kwa sura yake na utukufu wake akatawale na kumiliki vitu vyote viijazavyo dunia, mwisho wa mtu kutawala ni hapa duniani, mawazo ya ajira ni kutawaliwa bali mawazo yako ya kuajiriwa ni kujiandaa kusimamia ajira yak ohayo ni mawazo ya kibiblia ya kifalme, asili yetu ni kutawala na mtawala kazi yake ni kutoa hukumu kwa jina la Yesu kristo.
  Neno la mungu haliwezi kurudi bure ni lazima litimie hapa duniani. Kama alisema utawale ni lazima utatawala japokuwa watu wengi wameamua kujiita walokole, mtumishi, mkristo, mkristu, muumini kitu ambacho sio asili ya Mungu kuitwa hivyo. Asili ya Mungu ni Ufalme hapa duniani.
  Sheria ya Ufalme ni kwamba alichonacho Baba ni chakwangu naweza kukitumia maana mimi na Baba tunafanana ni haki yangu.
  Wakolosai 1:15

  Yesu ni mfano wa Mungu na sisi ni mfano wake tunamwita mfalme wetu. 
  Tafasiri ya Kuingia kwenye Ufalme wa Mungu kwa dhiki maana yake ni kutengwa na kunyimwa baadhi ya vitu kwenye familia au jamaa lakini ukivumilia utaingia na kufanikiwa. Ufalme wa Mungu kuingia kwa nguvu maana yake ni kuingia bila kujali kutengwa na upinzani wa familia au jamaa ambao wanakutukana na kukucheka na kukukebehi lakini ukingangania utaingia kwa nguvu na kufanikiwa.

  Ukiri
  “Mimi ni sura na mfano wa Mungu siyeonekana, mimi ni Mwana wa Mungu” 

  Shetani alimsumbua Yesu jangwani kwa kumwambia “kama wewe ni mwana wa Mungu”geuza mawe haya yawe mkate. Vita kubwa hapa duniani na ni silaha kubwa ya shetani ni kukufanya ujishuku asili yako, aliwafanya Adamu na Hawa wajishakie asili yao ili wale tunda wafanane na Mungu, shetani alijaribu kumfanya Yesu ajishuku asili yake kwa kujitupa chini lakini Yesu alimshinda.

  Mathayo 4:3
  Mathayo 8:29

  Neno Wakristo lililoanzia antiokia lililoanzishwa limegawanyika kwenye makundi mengi hapa duniani lakini halikutamkwa na Mungu.
  Mathayo 16:16

  Yesu alitaka kujua kama watu wanajua asili yake na ndipo Petro akamjibu kuwa yeye nii kristo mwana wa Mungu ndipo Yesu akasema juu ya mwamba wa Uwana wa Mungu aliye hai nitalijenga kanisa.

  Yohana 3:6, 4:24
  Mathayo 26: 61 – 66

  Yesu alikiri kuwa Yeye ni mwana wa Mungu na kwa wayahudi ukisema wewe ni mwana wa Mungu maana yake wewe ni Mungu. 
  Neno la lolote utakalolifunga kwa kigiriki linamaanisha lolote utakaloliruhusu hapa duniani kama mtawala na mbinguni wanasema endelea, hizo ndio funguo za Ufalme na tukiingia kwenye ufalme lolote tutakaloliruhusu mbinguni wameruhusu na ukiliamuru lisitokee mbinguni halitatokea. Wewe ni mfalme na lolote utakalolisema litatokea ukiwa na Ufalme wako ndani ya Ufalme.

  Yohana 10:30 – 37

  Yesu alimaanisha yeye na Baba wa mbinguni ni kitu kimoja. Unapokaa kimya bila kuzungumza sawa na asili yako unakuwa ni mfalme uliyepoteza Ufalme wako bila kujua. Wewe Mungu Baba, mwana na Roho mtakatifu wanakaa ndani yako halafu unabaki unalalamika bila kuamua kutawala hapa duniani na kumiliki, lengo la Yesu kuja hapa duniani lilikuwa ni kuja kutuletea Ufalme tulioupoteza.

  Kila kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu.