August 2, 2015

MAAJABU: MTUME ANAWALISHA WAUMINI NYWELE,NGUO NA NYOKA AKIDAI NI CHOCOLATE.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo watumishi na wahubiri injili wanazidi kuibuka na mafunuo mbalimbali ya huduma zao na kuacha maswali mengi kwa waumini wa dini ya Kikristo na wale wasioamini hadi kufikia kujiuliza kama miujiza ama maombezi wayafanyao wahubiri hao katika makanisa na huduma zao wamefunuliwa na Mungu. 

Wakati mwaka jana Afrika ya kusini iliibuka gumzo kwa muhubiri wake kuwalisha waumini nyasi pamoja na kuwanywesha mafuta ya petroli kwenye maombi BONYEZA HAPA. Kuna muhubiri mwingine wa huduma ya wanafunzi wa siku za mwisho iitwayo 'End Times Disciples Ministries' nayo ya nchini humo maeneo ya Tshwane ikiongozwa na mtume wake kijana Penuel Mnguni (24) ambaye amewalisha waumini wake nyoka akidai ni chocolate pamoja na kipande cha nguo alichofanyia maombi.

 Mtume huyo Mnguni ambaye amekuwa akiripotiwa na vyombo vya nchini humo kutokana na kuibuka na mbinu mpya 'za maombi' kila la leo. Kati ya maombi ambayo yamewaacha wengi wakijiuliza ni kuwalisha watu nyoka, nywele, nguo pamoja na kuwakanyaga waumini wake aina ya maombi ambayo hata mtume Lesego aliyewalisha waumini nyasi huwa pia anafanya. Ukiachana na vituko vya mtume huyo, swali limekuwa kwa utitiri wa waumini ambao wamekuwa wakimiminika kwenda kwenye maombi licha ya vituko vyote hivyo. 

Aidha kama msemo wa waswahili usemao 'ndege wa aina moja huruka pamoja' ndivyo ilivyo kwa mtume huyu kuelewana vyema na mtume Lesego wa manyasi ambapo amekuwa akitiwa moyo kusongesha mbele injili. KAZI KWENU WAPENDA MIUJIZA.
Mtume akimnyoa muumini wake ibadani


Alipanda mwanapunda eeh, hapana mtume akiwa mgongoni mwa muumini wake 

Mtume kijana Penuel akiwa amejituliza kwenye migongo ya waumini ambao "sitaki kuamini kama walikuwa hawajitambui". Mungu tusaidie.