• Isikupite Hii

  August 19, 2015

  NEWS: AKUTWA NA UMAUTI NYIKANI AKIJARIBU KUFUNGA KAMA YESU KWASIKU 40 BILA KULA CHOCHOTE.

  Picha ya Mlima Sinai unayoonekana kwasasa huko nchini Misri.

  Mwanaume mwenye miaka 73 aliyefahamika kwa jina la Reinfirst Manyuka kutoka Zimuto huko nchini Zimbabwe amefariki dunia baada ya kujaribu kufunga siku 40 bila kula chochote wala maji usiku na mchana nyikani kama alivyofanya Bwana Yesu wakati akijaribiwa na shetani.

  Kwa mujibu wa mtandao wa NewZimbabwe.com pamoja na Christian Post umeandika kwamba marehemu aliondoka nyumbani kwake june 15 mwaka huu nakuelekea jangwani ama mwituni ikiwa safari yake ya kiroho katika kujaribu kufunga kama alivyofanya Bwana Yesu. Kwa mujibu wa familia yake marehemu wamesema licha ya tukio hilo kumpata, marehemu alikuwa mtu mwenye imani na mamlaka safi katika Bwana na kwamba alikumbwa na umati sizaidi ya siku 30 bila ya chakula wala maji alipokuwa milimani.

  Taarifa zinasema Manyuka aliamua kuondoka nyumbani kwake ili apate wakati mzuri wa maombi ili kugeuza akili yake kumwangalia Mungu na kuondokana na tamaa za kidunia. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Polisi wa eneo la Masvingo inspekta Nkuleko Nduna ameuambia mtandao huo kwamba mwili wa Manyuka ulipatiakana vichakani mnamo July 15 ikiwa ni mwezi mmoja kamili toka alipoondoka nyumbani kwake. Aidha katika taarifa nyingine kutoka kwa familia ya marehemu inasema licha ya umri aliokuwa nao Manyuka bado alikuwa mtu mwenye afya njema na kwamba hakuwa na dalili ya kwamba angefariki ama yupo katika hatari ya kifo wakati anaondoka nyumbani.

  Hata hivyo licha ya taarifa kudai kwamba marehemu aliweza kufunga siku 30 bado uhakika wa kifo chake haujulikani kama alikufa kitambo nyikani kabla ya mwili wake kugundulika na mtu aliyetoa taarifa polisi au la. Ingawa inaonekana ni jambo la ajabu kwa mtu mzee kuondoka nyumbani kwake na kuelekea nyikani kufunga kwa zaidi ya mwezi, lakini kitengo chake kimekuwa kikikumbana na vifo mbalimbali vinavyotokana na watu kufunga bila kula chochote, lakini hatuwezi kuwazuia raia kufunga kwasababu ni jambo la kiimani alisema Inspekta Nduna.

  Aidha katika hatua nyingine kuonyesha kwamba waumini wengi hudhani kama wanaweza kuhimili kufunga kwa siku 40 bila chakula wala maji ni kwasababu ya mitume wengine ndani ya Biblia ukiachana na Yesu, kwenye kitabu cha Kutoka imeeleza kwamba Musa alifunga siku 40 bila chakula katika mlima wa Sinai kisha kupatiwa amri 10 za Mungu. Kama haitoshi baada ya kumshinda mtume wa Baali kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Wafalme mtume Eliya alifunga siku 40 bila chochote mpaka alipofikia mlima Sinai.