August 13, 2015

POWERFUL-SPEECH: SIRMBEZI AFUNGUKA, ASEMA MUZIKI WA INJILI SIO HUDUMA TU, NI KAZI NA BIASHARA PIA.


In fact I respect the fact that Gospel Music ni Huduma but I respect the fact that Gospel Music ni kazi, gospel music ni business kama tasnia zingine za Muziki na Filamu nk.

Gospel industry needs investments, ni tofauti na watu wengi wanavyoichukulia poa, kuanzia Sera za nchi na baadhi ya wadau 
Kuna watu/wadau/watumishi wanawanyonya waimbaji kwa kuforce mind zao ziamini kwamba gospel muziki ni huduma tu, Na tafsiri yao ya huduma ni kwamba is something you do, just doing(they say for God). Bila ya kujua kwamba atalipwa au atapata nini? yani ikimlipa sawa, asipopata pesa sawa..

Kwa upande wangu ningeeambiwa nitoe one word for gospel Music I would have said it is a business, typical business. Yaaani ni biashara ambayo watu wengi wanaichukulia poa, Hakuwezi kuwa na biashara kama hamna huduma, Hakuwezi kuwa na biashara kama hakuna fedha, Sijui watu wanaosema huduma wana maana gani? Huduma ya kuinvest muda, kipaji na pesa bila kujua hatima yake??

Tusiwe wajinga, Petro alimuuliza Yesu baada ya kuona kwamba Bwana hajatoa ahadi yoyoye ya kuvutia, Akaamua kumtolea uvivu na kumuuliza kwamba baada ya kuacha vitu vyote walivyokuwa wakifanya watapata nini?? Cha kushangaza ni kuwa Yesu hakumfukuza Petro wala kumfokea wala kumwita mpenda pesa, akampa jibu sawa sawa na swali alilouliza bila kupepesa macho kwamba kila mtu aliyeacha so and so atapata so and so.

Sir.Mbezi (Kushoto) Baada Ya Kupokea Tuzo.

Leo watu wengi wanawahimiza waimbaji kufanya kazi bila kujua hatma zao. Unaitwa ukahudumu huku haijulikani nauli yako inatoka wapi na mambo mengine ya msingi, Kuna waimbaji washaitwa mikoani wakaambiwa we njoo tuu utumike, na wakajua kila kitu ok. Akaogopa kuuliza kwamba mambo mengine yamekaaje akihofiwa kuambiwa mpenda pesa. Mwisho wa siku ya kurudi akapewa furushi la mihogo kama zawadi na kusindikizwa mpaka stendi, Akaachwa hapo na nauli hana mfukoni, ikabidi tu auze ile mihogo na simu yake ya mkononi apate nauli ya kurudi kwao.

Hakuna mwanadamu asiyekuwa na malengo, kila mmoja ana malengo yake na ana mikakati ya kuifikia, we ni nani uanyetaka kurudisha malengo ya wengine nyuma, unawezaje kusema uimbaji ni huduma tu unayofanya kwa ajili ya Mungu, Huku waendelea kujinufaisha wewe binafsi kupitia waimbaji.

We all know circumstance za kufanya kama huduma bila kutaraji kupata chochote, Katika kusaidia kufikisha injili kwa urahisi Zaidi, lakini sio ndio kasumba.

Kama unaandaa tamasha or whatever na unaweza kupata hela ya kutengeneza promotional Material kama posters, flyers uka print kwa kiwango kikubwa, ukalipia muziki, jukwaa, ma mc, transportation na kulipia matangazo radio, why not waimbaji??? na unaawaalika wengi ukijua ndio watakaovutia your targeted audience na bado wanatoka kapa..

Tena siku hizi kama ni kamuimbaji tu Fulani hakajulikani ndo kabisa no one wants you, Hata useme uko tayari kuimba free of charge siku zote, utaambiwa njoo nafasi ikiwepo utapanda
Hiyo ndio nitolee mwanangu, Angalau ukiwa na kajina kidogo ndo watakutafuta kidogoo na ukikaza ndo watakupa na ka nauli kidogo ambako wakati mwingine hakafikii total cost ya ulichotumia for them.

Ifike wakati wakati tuwekane wazi kwamba mwimbaji so and so naomba tusaidiane kufanya huduma ila hali ni ngumu na mazingira kabisa yawe yanaonesha ni ya kihuduma kweli maana siku hizi watu hawataki kukubali kwamba ili wote tuendelee lazima kuwe na mutual relationship, kila mmoja anufaike na kinachofanyika
Kama kila hatua ya kuandaa unachoandaa unalipia kwanini usimlipe anayefanya hilo tukio lako likafana??

Kama unafikiri muimbaji hapaswi kulipwa fikiria mara mbili,watu wanalalamika waimbaji wanafanya kazi mbovu kuanzia audio, video mpaka utumbuizaji bila kujua kazi nzuri zinahitaji uwekezaji
Na nitawekeza vipi kwenye kitu ambacho wewe unakichukulia for granted, muda wa kufanya mazoezi ya vocal, dancing, utunzi kwanini nisitafute kitu kingine ambacho kitanipatia kula na angalau kitanipa pesa ya studio angalau niwe na vijimbo viwili hata vya kuwaimbia play back.

Unataka kuniona kwenye kichupa (video) kikali unadhani namtoaje Alex Joseck marekani kuja kufanya video yangu, tushurkuru angalau Wana kingdom wamekuwa considerative kwenye gharama kwa kuwa wanaelewa tasnia ilivyooo.

Unataka niwe maarufu ndo angalau unialike au kunipa kitu kidogo, unajua ina cost how much japo kuapta promo ya wiki kwa radio?
Unajua gharama za kurekodi hata wimbo mmoja nab ado unataka niwe na album? Am not complain, am just saying I just wana see changes, nadhani hii inatokea Tanzania tuuu, maana ndio wenye uwezo wa kumualika muimbaji kutoka nje na kumpa lots of money na muimbaji mkongwe wa Tanzania wakamwambia Bwana akubariki, huh?? kwa kuwa kina Malope wao hawafanyi huduma eeh??

Pengine waimbaji wa Tz wamekuwa cheap sana, maana wao huimba tu bila kujua nini kinafuta, Hawana malengo kwenye maisha yao, may be wanadhani vipaji vyao walipewa bure kwa hiyo hawaitaji kupata pesa kupitia hivyo, au wana kiu saana ya kutumika mpaka kwenda sehemu ambazo hawajaalikwa 
Na kung’ang’ania kuimba na wakitoswa wanalalamika…where is professionalism??

Tasnia ya Muziki wa Injili itaendeleaa lini, labda kwa waimbaji wa live maana naona angalau wana sustain na kuimba kwenye stages ambazo ki ukweli angalau ziko advanced na kuna waimbaji na vikundi vina emerge lakini angalia upande huu wa solo artists toka walivyopaa kina Bahati, shusho, Rose, Bony na wengineo mwimbaji gani mwingine ameweza kuvuka hizo level ,no one
Tatizo wadau wengi wanapenda kunufaishwa na muziki wa Injili bila kuwekeza kwa waimbaji Na wengine wanahisi waimbaji wa injili kuingia mikataba na makampuni {endorsements) ni bonge moja la dhambi, wangependa kuona waimbaji wanaimba kanisani, kwenye mikutano na matamasha tu ambapo matamasha ya siku hizi yamepoteza ladha maana hamuendi tena kushuhudia mwimbaji akiimba bali akichangisha pesa ili atimize lengo lake na uimbaji huwa kwa sehemu ndogo tuuu, na lengo lenyewe mara nyingi halifikiwi maana atahadiwa pesa na mgeni rasmi kimbembe kukabidhiwa, atakopesha watu cd kwa lazima na hawatamlipa, aisee ni visangaa, tamasha lenyewe linaandaliwa kimagumashi tuu ratiba haileweki ,muimbaji aimbe, bado ashughulikiie muziki, sijui nini na nini..daaah kweli tunahitaji changes.

I think it’s time to welcome real investors kwenye muziki wa gospo, its time ya kuwalipa waimbaji when they deserve, Its time to go to the next level.