August 31, 2015

NEWS: TAG KILIMANJARO KUWAKOPESHA VIJANA PIKIPIKI (BODABODA).

Picha hii haiusiani na habari hii. Ni Picha tu ya pikipiki @bharathautos.

Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG), Jimbo la kilimanjaro limeanzisha mradi wa kuwakopesha vijana pikipiki ili wafanikiwe kibiashara.

Askofu wa jimbo hilo, Glorious Shoo alisema jana kuwa mradi huo utagharimu sh60 million.

Alisema pikipiki 50 zitanunuliwa na kukopeshwa kwa vijana hao ambao watapaswa kuzingatia sheria na kanunu za usalama barabarani.

"Baadhi ya vijana wanaoendesha bodaboda wamekuwa wakitumika katika vitendo vya uhalifu na kuongoza kwa kupata ajali. Tunataka kubadili mwelekeo huo mbaya, Vijana watakaokopeshwa ni lazima wapitie shule ya udereva na atakayezidisha makosa matatu ya usalama barabarani kwa mwezi atanyang'anywa pikipiki" alisema Askofu Shoo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, Joseph Mwakabonga alisema mpango huo ni mzura kwani vijana wengi wa bodaboda wanaweza kujifunza kutoka kwa vijana hao.

Source: Mwananchi