August 13, 2015

UKIFANYA MAKOSA HAYA (12) UTAHARIBU KURA YAKO.


1. Usijaribu kupiga kura zaidi ya mara moja.

2. Usijaribu kupiga kura baada ya muda kwisha.

3. Usijaribu kupiga kura kwa kutumia kadi ya mtu mwingine.

4. Usiweke kitu kingine zaidi ya karatasi ya kupigia kura katika sanduku la kuhifadhia kura.

5. Usichane orodha ya wapiga kura au mabango yoyote ya elimu kwa mpigakura.

6. Usighushi au kuharibu karatasi ya kura.

7. Usichapishe na kusambaza karatasi za kura bila mamlaka kisheria.

8. Usipokee au kutoa rushwa kabla na wakati wa uchaguzi.

9. Usimzuie mwingine kupiga kura kwa uhuru na amani.

10. Usitoe siri ya kiongozi aliyepigiwa kura na yeyote.

11. Usiweke alama yoyote ya utambulisho katika karatasi ya kura.

12. Usivae au kuonyesha alama yoyote ya chama wakati wa upigaji kura.

Source: Mwananchi.