August 7, 2015

SOMO: WANATAFUTA KILICHONDANI YAKO - ASKOFU GWAJIMA.


Waganga wakienyeji, wachawi na wasomanyota, na shetani mwenyewe wanapokufuatilia usifikiri wanatafuta surayako au malizako, tambua kuwa wanatafuta kilichoko ndani yako ulichowekewa na Mungu. 

Kimsingi, watu wengi ambao Mungu aliwaita walikuwa na matatizo makubwa kabla ya kile walichopangiwa na Mungu kutokea. 

Na hata wewe vita ulivyo navyo ni kwakuwa wanatafuta kilichoko ndani yako ulichopewa na Mungu wakiharibu. Yakupasa ujue wewe kuwa ni rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita, mwali wa moto, chumvi ya ulimwengu, nuru ya Ulimwengu, Mwanafunzi wa Yesu na zaidi ya yote wewe ni mwana wa Mungu na hivi ndivyo ulivyo na shetani na mawakala wake hapendi ujitambue hivi na kufahamu vitu vilivyoko ndani yako amabavyo washirikina wanatafuta ili kuviaharibu, na ndivyo vinawatisha, vinawafanya wakuwinde usiku na mchana ili kukiharibu kile ambacho Mungu ameweka ndani yako. 

Imeandikwa,
Mwanzo 37:17-32
“Yule mtu akasema, wametoka hapa, maana niliwasikia wakisema,Twendeni Dothani BasiYusufu akawafuata nduguzake akawakuta huko Dothani, Wakamwona tokea mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana waokwawao, tazama, Yule bwana ndoto anakuja”.
Adui anaweza kukuona toka mbali akafanya shauri la kukuangamiza. 

Mfano ndugu zake Yusufu walipo muonaYusufu walisema ‘bwana ndoto Yule anakuja’. Kumbe ukionekana kile kilicho ndani yako watu waweza kufanyia shauri baya juu yako na kukubadilishia jina lako. Wachawi na waganga wa kienyeji na mawakala wengine wa shetani waweza kumuona mtu kwa mbali au kuona kilichoko ndani yako kabla hata ya kuzaliwa ukiwa bado tumboni mwa mama yako, na lengo kuu ni kusimamisha kilicho kondani mwako ambacho Mungu amekuwekea.

Imeandikwa,
Kutoka 1:15-22
“Kisha mfalme wa misri akasema na wazalisha wa waebrania, mmoja jina lake aliitwa shifra, na wapili aliitwa Pua, akasema, wakati muwazalishapo wanawake wa kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwani mototo mwanaume, basimwueni, bali ikiwa ni mototo mwanamke na aishi.”

Katika hali ya kutaka kuwaua watoto wa kiyahudi jambo hili lilikua linawalenga wachache akiwemo Musa maana wenye nia mbaya wana uwezo wa kuona tokea mbali kusudi aliloliweka ndani ya Musa. 

Na jambo hili si kwa namna Musa alivyoonekana usoni, bali ilikua ni kwasababu ya kile kilichoko ndani mwake. Haikua rahisi Musa kukaa mtoni na asiliwe na mamba au asisombwe na maji, bali ni kwakuwa Mungu alikuwa anampango na Musa. Mungu anauwezo wa kulinda mpango wake kwa gharama zake mwenyewe, na haitaji msaada wa kulinda mpango wake.

Usijione wewe kama hunakitu, Hapana wewe kunavitu vilivyopandwa na Mungu ndani yako, amabavyo hakuna mtu anayeweza kuviondoa, na vimepandwa kwa makusudi na Mungu kwa wakati wake na kwa makusudi yake.

Mashetani wana uwezo wa kuona vitundani ya watu tokea mbali, mfano Gideoni, Paulo, Samsoni, hawa walikua ni watumishi wa Mungu amabao hawakujulikana kwa namna ya usoni lakini matendo yao kabla ya kufanyakazi ya Mungu ilidhdihirisha kilichokuwa ndani yao na ndiomaa na kwa mfano mtume Paulo shetani alimtumia sana katika kuwaua watumishi wa Mungu kwa makusudi ili kumpeleka mbali na kile ambacho Mungu amepanda ndani yake, lakini wakati wa Mungu ulipofika mtume Paulo alipo okoka akanza kuifanya kazi ya Mungu na ndio mtume pekee aliyeandika vitabu vingi kuliko wote juu ya ufalme wa mbinguni.

WACHAWI WANAWEZA KUKUJUA WEWE NA KILICHOKO NDANI MWAKO

Mashetani walimtambua Yesu kuwa ni mtakatifu wa Mungu, Mwana wa Mungu.
Imeandikwa;
Luka 4:34
“Akisema, Acha tuna nini nawe, Yesu wa nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nan, Mtakatifu wa Mungu.”
Matendo 19:15
“Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjuana Paulo namfahamu,lakini ninyi ni nani?”
Marko 1:24-26
“AkisemaTunanini nawe, Yesu wa nazareti? Je? Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa umtoke. Yulepepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwasauti kuu, akamtoka” 
Ufunuo 12:12-17
1. Shetani anauwezo wa kuona kilichoko ndani mwako.
2. Shetani alikua ameona Yusufu atakavyoku wakiongozi katika nchi ya Misri.
3. Shetani pia aliweza kujua jinsi Yusufu atakavyo wasaidia nduguzake wakati wa njaa.
4. Wale wale waliopanga mpango mbaya juu yako njaa itawapata na watakuja kwa upole kusujudu mbele zako. Na wewe usiwafanyie mabaya wape chakula wale. Ujiulize kwanini wewe unaye enda kanisani ndio unarogwa kuliko hata watu wengine? Wachawi wanaiona kesho yako mapema ndomaana kila eneo lenye hatima ya mtu ndilo lenye vita kubwa sana. Yakupasa usimame kwenye kusudi la Bwana.

Shetani hapambani na kitu kisicho na madhara kwake. Ndoto mbaya, magonjwa na shida zinazokukabili ni ili kile kitu kilichoko ndani mwako kisitendekazi.
Maombi;
“Baba Mungu katikajina la Yesu, naomba unioneshe kitu ulichokiweka ndani mwangu. Naamuru ile hatima iliyoko ndani mwangu itokee kuanzia sasa katika jina la yesu.”
Unaweza ukawa umewekewa na Mungu kitu kikubwa ndani yako na usikigundue au usitambue Mfano; Yohana hakujua yeye ni nani alijuatu kuwa yeye ni Sauti ya mtua liaye nyikani.

Kuna mambo yaliyofichwa machoni pako, yawezekana ukishafika mbinguni ndio utatambua wewe ulitakiwa uwe nani hapa duniani.
Kwenye ulimwengu wa roho hakuna umbali, na mashetani wanaweza kuzuia kwasababu ya woga wakile kitakachotokea. Mfano, Daudi alijulikana anaweza kumuua Goliati kabla haja zaliwa. Hawashindani na wewe kama mtu bali wanashindana na hazina iliyoko ndani yako. Inawezekana wanakuona wewe utakua na familia nzuri, utamiliki kampuni au utakuwa kiongozi mkubwa na kupata mafanikio ndiyo maana ya vita ulionayo.
Maombi; 
“kwajina la Yesu mashetani wote walitumwa juu yangu kuharibu hatima yangu au kuharibu kile ambacho Mungu alichokiweka ndani mwangu nawasambaratisha kwa jina la Yesu. Naamuru kila jini, balaa, mikosi iliyoko ndani mwangu iniachie kwa jina la Yesu.”

MASHETANI NA WACHAWI WANAWEZA KUFANYA KAZI KWA NAMNA TOFAUTI.

1. Mashetani na majini wanaweza kuingia ndani mwako
2. Mashetani na majini wanaweza kukaa nje na wakakuongoza kufanya kitukibaya hata kama hupendi. Zakaria3:1
Kuna watu wanakuona hatima yako kazini ndiyomaana unakuwa mgonjwa na taabu nyingi katika eneo la kazi.

Wewe unajiona una matatizo yanayokufuata na huelewi kwanini yanakufuata. Kile Mungu alichokiweka ndaniyako ndocho kitakacho fungua milango ya mafanikio yako. 

wachawi, waganga wakienyeji na wasoma nyota na washirikina wanatafuta kukunyanganya ulichopewana Mungu. Kwa mfano Kinachomfanya mtu ale vizuri na kufurahia maisha ni tofauti na kile kilichokupa ufaulu wa masomo shuleni kwa maana hiyo Elimu haimwakikishii mtu mafanikio bali inamsaidia kufungua mlango wa kuendeleza kile kilichoko ndani yake alichopewa na Mungu. Na ukishinda rohoni lazima mwilini mambo yaende sawa. 

Mambo yako kwenda sawa hakutegemei kiwango cha fedha ulicho nacho.
Watu wengine wanaweza kuchukua mikono ya mtu na kufanyia kazi kama biashara wakatajirika, huku mwenyemikono akawa maskini kupindukia kwanamna ya kichawi hivyoni vizuri kujifunza na kufahamu mbinu za shetani na mawakala wake na kuzivunja na kuzishinda kazi zao kwa jina la Yesu..
Maombi;
Kila hatima ya mtu iliyoibiwa irudisha kwa jina la Yesu. Majini wote, balaa zote nazisambaratisha kwa jina la Yesu, pokea Roho ya uzima katika jina YESU KRISTO. Amen.

Source: Gospel Kitaa