September 10, 2015

NEWS: MCHUNGAJI ALIYEKATAA KUTOA CHETI CHA NDOA KWA MASHOGA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA.

Mchungaji Kim Davis

Hatimaye mchungaji aliyewekwa lupango kwa kosa la kukataa kuwapa kibali cha ndoa wapenzi wa jinsia moja huko Kentucky nchini Marekani, ameachiwa huru na mahakama hapo jana na kuahidi kurejea katika utumishi wake wiki hii.

Mchungaji Kim Davis alimwaga machozi mbele ya kundi kubwa la wafuasi waliokuwa wakiunga mkono msimamo wake, ambapo aliwashukuru kwa upendo wao waliouonyesha, sambamba na kuwaambia kuwa anarudisha utukufu kwa Mungu kwa umoja na ukakamavu waliouonyesha, na kuongeza kwamba wanamtumikia Mungu aliye hai na kwamba anawajua kila mmoja kwa nafasi zao, kwakuwa yeye ni Mkuu.

Mchungaji Davis alionyesha msimamo wa kuwa tayari kwenda jela maisha kuliko kuhalalisha ndoa ya watu wa jinsia moja kwakuwa ni kinyume na imani pamoja na dini yake. Akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kama kukaa kwake jela kuna mafanikio yeyote, mchungaji huyo alijibu kwa tabasamu huku akitingisha kichwa akimaanisha mafanikio yapo.

Kwa upande wa mwanasheria wa mchungaji huyo Mat Staver amesema mteja wake atarejea kazini wiki hii na kwamba hata jiuzulu nafasi yake. Hata hivyo mchungaji Davis hakuweka wazi kuhusu kesi yake, huku maswali kuhusu tukio hilo yakiwa hayajibiwa lini ataanza rasmi kazi na ni kitu gani atakifanya atakaporejea kazini kwake.

Mchungaji Kim Davis aliwekwa jela na jaji David Bunning ikiwa siku tano tangu jaji huyo kumuhukumu mchungaji huyo kwenda jela, ambapo aliachiwa sambamba na kupewa masharti ambayo mchungaji huyo hayuko tayari kuyakubali. Aidha taarifa zinasema, jaji huyo aliridhishwa na hatua ya kumwachia mchungaji huyo kwasababu wafanyakazi wenzake walitoa kibali cha ndoa kwa wapenzi hao ilihali mchungaji Kim Davis akiwa jela.Mmoja wa watu waliokuwa wakiunga mkono msimamo wa mchungaji Davis akiwa na bango la kutaka mchungaji huyo kuachiwa huru.

Tazama video chini namna mchungaji Kim Davis alivyoonyesha msimamo wake kwa mashoga hao kabla hajakamatwa.