Featured Posts

September 11, 2015

NEWS: MWINJILISTI AUWAWA KWA KUCHOMWA MISHALE.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani.

Mwinjilisti wa Kanisa la Waadiventisha Wasabato, Yese Mileyi (50) ameuwawa kwa kuchomwa mishale miwili na watu wasiojulikana ambapo mshale mmoja ulimpata shavuni na mwingime mgongoni  na kufariki dunia hapo hapo.

Tukio hilo lilitokea Septemba 8 mwaka huu majira ya saa 1:14 jioni katika Kijiji cha Mahando  mterini, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro .

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwinjilisti huyo alikuwa anatokea shambani kuelekea nyumbani na kuchomwa  mishale hiyo na watu wasiojulikana na kusababisha kifo chake.

Kamanda alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma , huku jeshi la polisi likiendelea kuwasaka waliofanya mauaji hayo.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limewataka wananchi wa Moshi kufanya siasa za amani  na utulivu na kuacha kuchana  picha za wagombea walizo zibadhika katika sehemu mabalimbali za mkoani humo.

Kamanda Ngonyani alisema kumekuwapo na matukio mengi yanayoripotiwa na wagombea wakiwashutumu baadhi ya wananchi kuchana mabango pamoja na picha za wagombea.

Source: Mwananchi.