October 6, 2015

EXCLUSIVE: DA' T.R.U.T.H. ATANGAZA JINA LA ALBUM YAKE MPYA.


Kupitia mitandao ya kijamii, Mwimbaji wa muziki wa injili wa kizazi kipya nchini marekani "DA' T.R.U.T.H", ametangaza mipango ya kuachia album mpya, ambayo itakuwa ni album yake ya nane tangu aanze kufanya muziki wa kizazi kipya yani Gospel Hip Hop.

DA' T.R.U.T.H moja kati ya waanzilishi wa muziki wa Gospel Hip Hop, aliweka wazi kupitia account yake ya Instagram kwamba album hio itakwenda kwa jina la " IT'S COMPLICATED". Album yake ya awali "HEART BEAT" ilishika nafasi ya "84" Billboard 200, pia ikashika nafasi ya "2" katika album za nyimbo za injili na "8" katika Rap albums.