October 30, 2015

HASIRA NI HASARA KWA AFYA YAKO? (SOMA HAPA)


Je unajua kama hasira inaweza kukusababishia mshtuko wa moyo au kiharusi?

Watafiti Nchini Marekani wamebaini kuwa tendo la kupandwa na hasira mbaya linaweza kuchangia hatari kubwa ya mtu kupatwa na mshtuko wa moyo ama ugonjwa wa kiharusi.

Hasira huja kabla ya mtu kupatwa na mshtuko wa moyo na pia inaweza kuwa sababu kuu ya mshtuko huo.

Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa waliweza kutambua kipindi hatari ambapo kwa masaa mawili wakati watu walikuwa katika hatari ya kupatwa na mshtuko wa Moyo.

Lakini wanasema kuwa utafiti zaidi unahitajika kuelewa kwa undani, uhusiano kati ya hasira na mshutuko wa moyo na ambavyo inaweza kuzuiwa.
Haijulikani kinachosababisha athari hii. Inawezekana labda inahusishwa na mabadilko ya kisaikolojia ambayo hasira inasababisha kwa miili yetu, lakini utafiti zaidi unahitajika.

Watu ambao wako katika hatari ya kukumbwa na hali hiyo ni wale ambao labda wanatoka katika familia yenye historia hiyo.

Mmoja wa madaktari waliohusika na utafiti huo, Daktari Mostofsky alisema kuwa , "ingawa tisho la kukumbwa na mshutuko wa moyo kutokana na kiwango kidogo cha hasira ni ndogo sana , tisho linaweza kuwa kubwa kwa watu wenye kupata hasira mara kwa mara.

Haijulikani kwa nini hasira ni hatari , watafiti wanasema kuwa matokeo yao hayathibitisha wazi ikiwa maradhi ya moyo pamoja na tatizo la Damu kuzunguka mwilini yanasababishwa na hasira.

Wataalamu wanasema kuwa shinikizo la mawazo pia linaweza kusababisha tatizo la moyo, hasa kwa sababu linapandisha shinikizo la damu lakini pia kwa sababu watu wanaweza kukabiliana na shinikizo la mawazo kwa njia tofauti ambazo sio nzuri kwa afya mfano kwa kuvuta sigara au kulewa.

Watafiti hao wanasema kwamba ni muhimu kuchunguza ikiwa mambo yanayoweza kuzuia shinikizo la mawazo yanaweza kuzuia athari hiyo kwa Moyo.