Featured Posts

October 7, 2015

NEWS: MCHUNGAJI AFUTA IBADA SIKU YA KUPIGA KURA OKTOBA 25.


Mchungaji wa Kanisa la Ufunuo maarufu Mungu wa Bendera wilayani Bukombe Mkoa wa Geita, Heriyabwana Majebele amesema Oktoba 25 hakutakuwa na ibada kanisani hapo, badala yake waumini waende wakapige kura.

Alisema Ibada Kuu itafanyika Oktoba 23. “Oktoba 25 ni siku ya kuheshimiwa na kukumbukwa katika historia ya Tanzania, ni siku ambayo tutapiga kura kwa ajili ya kuwapata viongozi wa nchi yetu, kama mchungaji wenu, ninafuta Ibada Kuu siku hiyo ili niwape nafasi ya kwenda kuifanya kazi hiyo,” alisema Mchungaji Majebele kanisani hapo Jumapili iliyopita.

Aliwataka waumini kuachana na vishawishi vya makundi ya kuanzisha vurugu bali wakimaliza kupiga kura warejee nyumbani kuendelea na shughuli zingine za maendeleo huku wakisubiri kutangazwa kwa matokeo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mchungaji Majebele alisema kiongozi bora hutoka kwa Mungu, waumini wa kanisa hilo na Watanzania kwa ujumla, hawana budi kuiombea nchi amani ili uchaguzi huo upite salama.

Source: mwananchi.