October 23, 2015

UNACHOPASWA KUFANYA SIKU YA KUPIGA KURA.


Kupiga kura ni suala linawaunganisha na kuwahusu Watanzania wote, hakikisha unaenda kupiga kura ili umchague rais, mbunge na diwani, ambae anafaa kuwa kiongozi wako kwa miaka 5 ijayo. 

•Fika katika kituo cha kupigaji kura katika muda uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambao ni kati ya 1:00 asubuhi hadi 10:00 jioni.

•Baada ya kupiga kura unatakiwa kuondoka eneo la kupigia kura

•Usifanye kampeni ya aina yoyote siku hiyo.

•Usivae sare zinazokutambulisha kuwa wewe ni mfuasi wa chama chochote cha siasa.

Source: Mwananchi,