October 2, 2015

EXCLUSIVE: UJAUZITO WAMPELEKEA GOSPEL RAPA KUIKIMBIA RECORD LABEL.


Rapa Heesun lee, Mwanadada wakimarekani wenye asili yakikorea, anaefanya vizuri kabisa katika muziki wa hip hop (Gospel), hivi karibuni aliamua kuondoka na kuachana na Record Label aliokuwa akifanya nayo kazi "In My City Records", na kuwa Msanii wakujitegemea. Baada ya Rapa huyu kuhojiwa na moja kati ya mitandao mikubwa ya muziki wa Gospel Hip Hop Nchini Marekani "Rapzilla.com".

Alisema "Mimi na Record Label Hii tulikuwa na matatizo tofauti yakiufundi, na nikaona nibora tu niondoke. Na sababu kubwa ni kwamba mimi natamani kupata mimba na nizae mtoto wingine, hili swala limekuwa tatizo kwa muda mrefu tu, Nilitamani kurecord nyimbo nyingi sasa ambazo zita-cover kipindi chote cha ujauzito, Lakini mpaka sasa hakuna wimbo hata mmoja nilio-record."