October 27, 2015

UCHAGUZI WAVUNJA NDOA ZA WATU.


Hii ilitokea Zanzibar jana, ambapo mume na mke walipishana, mume alikuwa na mapenzi juu ya chama kingine na alikuwa anakitaka hicho chama chake tu na mke naye alikuwa na mapenzi juu ya chama kingine na alikuwa anakitaka chama chake tu. 

Mwisho wa mzozo wao ilikuwa ndoa kuisha kwenye Kituo cha kupiga Kura, mume akachukua kalamu na karatasi na kuandika talaka hapohapo !!

Kisa kingine kimetokea Mwananyamala Dar ambapo mmoja wa wasimamizi alihisiwa ameenda chooni kuficha karatasi za Kura, baadae watu waliokuwa kwenye foleni walimletea mzozo lakini baada ya Askari kuingilia kati walichunguza na kugundua hakukuwa na ukweli wowote kuhusu Msimamizi huyo kuficha Kura.

Source: MillardAyo.

Sikiliza hapa.