October 24, 2015

NI SHERIA GANI INAYOKURUHUSU KUFANYA MAMBO YASIYOWEZEKANA? (HII HAPA)


Sheria pekee inayokuruhusu wewe Mkristo kufanya mambo yasiyowezekana ni sheria ya miujiza. Miujiza hutendeka kupitia jina la Yesu, kwa nguvu inayotoka katika ulimwengu uliofichika ambako Mungu huketi (Mbinguni), kupitia roho ya mwanadamu, ambayo ndio kiini cha ubinadamu wetu, kupitia akili ya mwanadamu, huku ambako wakati mwingine mashaka huanzia, na kisha kutoka nje duniani (kudhihilika) kupitia mawazo na maneno tunayotamka.

Lakini hali hii ya mashaka lazima itiliwe mkazo. Ukisoma (Marko 11:22-24) inazungumza kuhusu imani na mashaka . Mtu mwenye mashaka hato pata lo lote toka kwa Bwana (Yakobo 1:6-8).

Yesu alisema "Nanyi mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea ili Baba yenu wa mbinguni apate kuwasamehe ninyi makosa yenu.  Lakini msipowasamehe wengine, basi makosa mliyofanya ninyi hayatasamehewa na Baba yenu wa mbinguni." Marko 11:25.

Kipingamizi kikubwa cha miujiza ni ukosefu wa msamaha. Lazima mtu awe huru kutoka katika uchungu, wivu na chuki, nje ya hapo hakutakuwa na miujiza ya kuamisha milima. Ili tuone miujiza ikifanyika katika yetu kama wakristo lazima msamaha na upendo viwepo.