Featured Posts

October 20, 2015

Je wajua kwamba mwaka 2013 Christina Shusho alichukua tuzo gani huko London? (soma hapa).

Nyota wa muziki wa gospel nchini mwanadada Christina Shusho alitwaa tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike mwaka 2013 katika tuzo za Africa Gospel Music Awards zilizofanyika katika ukumbi wa The great hall chuo kikuu cha Queen Mary jijini London nchini Uingereza.

Christina Shusho alipata tuzo hiyo katika kinyang'anyiro cha waimbaji wapatao tisa kutoka Kenya pamoja na Uganda huku Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na waimbaji wawili, Christina Shusho pamoja na Martha Mwaipaja.