October 3, 2015

Utajiri wa Tb Joshua waiacha serikali ya nchi yake hoi.

Mchungaji wa Kiongozi wa makanisa ya ‘Synagogue church of all nation’ TB Joshua, ameingia kwenye ‘list’ ya wachungaji wachache wanaomiliki ndege binafsi barani Africa.

TB Joshua mwenye maskani yake nchini Nigeria, ametoa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 60 ili kumiliki ndege hiyo aina ya Gulfstream G550. Kwa mujibu wa kituo cha Habari cha Sahara, stakabadhi ya ununuzi wa ndege hiyo ulifanyika tangu mwezi wa nne mwaka huu.

Taarifa za ndani zaidi zinadai TB Joshua, mwanzoni aliletewa ndege hiyo mwezi wa 12 mwaka 2013 kwa ajili ya kuiona ili akiridhika nayo utaratibu wa manunuzi ufatwe.

Serikali ya Nigeria imepanga kufanya uchunguzi kubaini mapato kamili ya kanisa la mchungaji huyo.