October 27, 2015

MADHARA 7 YA HOFU YA KUTOA ZAKA ZETU KWA BWANA - PASTOR MITIMINGI.

Mchungaji Peter Mitimingi.

MADHARA 7 YA HOFU YA KUTOA ZAKA

1. Hofu hutujengea mazingira kwamba nikitoa zaka huenda nitapungukiwa.
2. Hofu hututishia kwamba ukitoa zaka hutaweza kumaliza mwezi huu.
3. Hofu hutusababishia kutochukua hatua ya kubadilika na kusonga mbele.
4. Hofu hutufanya kuwa watumwa wa madeni na umaskini wa kudumu.
5. Hofu huharibu uhusiano wetu na Mungu 
6. Hofu Hii Hutukosesha kuzipata Baraka za Mungu Kwetu
7. Hofu hii Hutufanya tuwe na maisha ya mifuko iliyo toboka sikuzote. Tunapata sana pesa lakini hazikai.

ULIPE DENI LA ZAKA UNALO DAIWA NA MUNGU SASA!

  • Malaki 3:8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu

HATUMPI MUNGU BALI MUNGU ANATUPA SISI.

Maandiko yanasema, “Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea. (1Nyakati 29:14). Mungu ni mkarimu sana kwetu. Hutupatia asilimia tisini (90%) na huhitaji tena asilimia kumi tu (10%) ya vitu ambavyo ni haki yake. Je! Fikiria kama Mungu angekuwa mbinafsi na akaagiza kwamba kila mtu amtolee 90% ya mapato yote na ile 10% ndiyo abaki nayo kwa matumizi yake na familia yake. Hapo sijui hali ingekuwaje! Nadhani makanisa mengi sana yangekuwa matupu kutokana wengi kushindwa kutimiza sharti hili.