November 2, 2015

CHRISTINA SHUSHO NI MMOJA WA MABALOZI WA AMANI NCHINI.

Christina Shusho
Siku chache zilizopita, Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Bi. Christina Shusho amekuwa ni mmoja kati ya wanamuziki walioteuliwa kuwa mabalozi wa amani nchini kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Nimezipata habari hizi kupitia ukarasa wa facebook wa mwanamuziki muimba mashairi, Mrisho mpoto aliyendika kama ifutavyo.

"Ni nafasi ya kipekee na heshima kubwa kupitia ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania, kututeua mimi na Christina Shusho kuwa mabalozi wa amani Nchini. "Amani yetu fahari yetu" nyuma ya neno hili kuna maisha ya watanzania. Wanasisa wetu wapenzi najua mmejaliwa nguvu ya ushawishi, nawaomba tumieni karama zenu mlizopewa na Mungu kuihubiri amani kipindi hiki, maana nyuma yenu kuna wototo yatima, wazee na watu wenye mahitaji maalumu. ni kweli kuna maisha baada ya uchaguzi, ningeomba tena kwa unyenyekevu yawe maisha yenye amani. Watanzania wenzangu tuepuke Siasa za chuki na makundi, zinaweza kuhatarisha amani yetu. ‪#‎Unduguwetuuendelee‬ ‪#‎amaniyetufahariyetu‬."