November 6, 2015

SIO GOSPOMUZIKI.COM TENA. SASA NI GOSPOMEDIA.COM. KWA NINI? (SOMA HAPA)


Moja kati ya Kampuni bora hapa nchini inayosapoti Muziki wa Injili pamoja kusambaza kazi za waimbaji, wachungaji, wajasiriamali na waandishi wa articles mbalimbali kupitia mtandao, Wamebadilisha jina la kampuni yao kutoka www.gospomuziki.com kwenda www.gospomedia.com.

Baada ya kuongea na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo Mh. Aloyce Mbezi maarufu kama Sirmbezi alisema "Ndio ni kweli tumebadilisha jina la kampuni yetu, tunaomba radhi kwa wadau wetu wote kwa usumbufu huo, Lakini sababu iliyotupelekea kubadilisha jina la kampuni yetu kutoka www.gospomuziki.com kwenda www.gospomedia.com ni kwa ajili ya kupanua wigo na kuboresha huduma zetu tunazozito kwa jamii".

www.Gospomedia.com