November 4, 2015

NEWS: MTUMISHI WA MUNGU TB JOSHUA AMEKUJA TANZANIA.

TB Joshua akiwa na Rais Kikwete. 

Mhubiri wa kimataifa wa Kanisa la Church of All Nations  lililopo Nigeria, TB Joshua ametua Dar leo. 

Mara baada ya kutua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu. Julius k. Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete.

Ripota wa millardo.com aliandika habari katika tovuti hiyo na kusema kwamba "TB Joshua amekuja kama mmoja ya wageni watakaoshuhudia tukio hilo la kuapishwa kwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania."