November 4, 2015

MAAJABU: MTOTO ALIEZALIWA BILA SEHEMU YA KICHWA NA UBONGO, ATIMIZA MWAKA (VIDEO)


Jaxon Buell alizaliwa August 27 2014 huko Birmingham, Uingereza akiwa hana sehemu kubwa ya fuvu la kichwa pamoja na ubongo.

Madaktari waliligundua tatizo la huyu mtoto tangu kipindi ambacho bado hajazaliwa, Brandon na Brittany ambao ni wazazi wake walishauriwa na Madaktari kwamba ni bora ujauzito wake ukatolewa… wao hawakukubali, kingine kikafuatia kwamba hata akizaliwa,hatokuwa na maisha marefu atafarariki kutokana na ukubwa wa tatizo lake.

Baada ya miezi mingi kupita akiwa anafanyiwa uchunguzi na madaktari waligundua kuwa hakuna kinga yoyote itakayomsaidia kuendelea kuishi lakini wazazi wake hawakukata tamaa na walifanya kila jitihada kuhakikisha mtoto wao anaendelea kuishi.


Wazazi wa Jaxon, Brandon na Brittany pamoja na mtoto wao wakiwa na nyuso za furaha

Wazazi hao waliweza kukusanya kiasi cha dola 100,000 kutoka kwa watu mbalimbali ili kuokoa maisha ya mtoto wao tangu azaliwe na sasa ana miezi 13 na anaendelea vizuri.

Video hii hapa.