November 6, 2015

NEWS: MAJAMBAZI WAPORA HUKU WAKIIMBA 'HAPA KAZI TU'.

picha hausiani na habari hapo chini

Kundi la watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbalimbali kama mapanga na marungu, juzi waliteka magari katika kijiji cha Igogo kata ya Nanga Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora huku yakiimba ‘Hapa kazi tu.’

Baadhi ya madereva waliokumbwa na janga hili, walidai kuwa baada ya kusimamishwa na majambazi hao, waliwashambulia kwa marungu na bapa za mapanga wakiwaamrisha watoe fedha na simu za mikononi huku wakitamka kila wakati kaulimbiu iliyokuwa ikitumiwa na Dk. John Magufuli 
"Hapa Kazi tu". 

Walisema majambazi hao walifanikiwa kuwapora madereva zaidi ya Sh. milioni mbili taslim.

Source: East  Africa  radio