November 6, 2015

EMMANUEL MBASHA AZUNGUMZA KUHUSU NDOA YAKE NA FLORA. (+AUDIO)

Emmanuel na Flora Mbasha kabla hawajatengana
Ni zaidi ya mwaka mmoja umepita tangu wawili hawa hawako kwenye ndoa yao, Emmanuel pamoja na Flora Mbasha. Vitu vingi vimepita hapo katikati ikiwemo ishu ya kesi za Mahakamani.

Ndoa yao itarudi baada ya kuisha kwa kesi ya madai ya talaka? Emmanuel amesema inahitaji muda wa kukaa na kutafakari kabla ya kuamua chochote kwa sasa.

Emmanuel Mbasha amesema japo walikuwa kwenye kambi mbili tofauti kwenye Kampeni haimaanishi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote iliyofanya wasirudiane. Emmanuel alionekana na Dokii kwenye Kampeni lakini anasema kila mmoja ana maisha yake, hakuna chochote kilichoendelea kati yao.


Sikiliza Hapa chini


Source: Millard ayo & Soudy Brown.