November 12, 2015

EXCLUSIVE: KUTANA NA SIRMBEZI AKIELEZEA KUPANDA NA KUSHUKA KWA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.


"Wapo wanahoangahika ndani hadi nje ya nchi kufanya video zenye ubora zaidi wengine wanaamini kufanya video yenye gharama kubwa ni anasa.

Wakati wengine wanashinda kwenye mazoezi ili kufanya performance nzuri wengine wanasubiri siku ya perfomace ifike abebe CD yake aimbe kisha airudishe kuifungia mpaka perfomance ijayo.

Wakati wengine wanahaha kufanya event management nzuri, kuweka stages nzuri, lights nk, wengine wanasema Bwana anashuka popote hata mchangani(ni kweli lakini)

Wakati bloggers wengine wanahaha kutafuta contents za habari kwa usahihi wa hali ya juu kuna wimbi kubwa la bloggers ambao hawajui A wala B.

Wakati wengine wanawaza kufanya muziki wao International wengine wanasema International kitu gani,ishu uswazi(wote wako sahihi)

Wakati wengine wanatafuta kufanya audio zenye ubora, wengine studio yoyote twende kazi ili mradi maneno yanasikika watu wataguswa (ni kweli lakini)

Wakati wengine wanajaribu kubuni vitu vipya zaidi, miondoko, melodies nk, wengine wansema haijalishi ili mradi ukiwa umejaa roho hata ukiimba off key watu wanadaka (ni kweli lakini)

Wakati watangazaji wengine wanapigania muziki wa injili upate rotation kwenye media, wengine kama huna laki 2 usiwasogelee

Wakati kundi kubwa la waimbaji wakihemeaa kujenga fanbase kwenye social networks, wapo wasiotaka kusikia habari za za hii mitandao wanayoiita ya ki free mason.

Wakati waimbaji A wanatoa ushirikiano kwenye mambo mbali mbali,waimbaji B wanaleta mapozi na kujiona "no one like them"

wakati waimbaji wenye wito wanahangaika na Mungu usiku na mchana ili wamtumikie kwa roho na kweli,kina wimbi kubwa la waimbaji ambao ni wapigaji,usiingie kwenye 18 zao.

Haishangazi kuona radio za secular zina updates nyingi za gospel kuliko radio za gospel.

haishazi kuona hakuna vipindi vinavyoruhusu wasikilizaji ku request nyimbo,hata vikiwepo ni geresha,rotation ni ile ile.

haya machache na mengineyo nisiyoyajua, ongeza na lako" Alisema Sirmbezi kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Toa Maoni Yako Kwa Kucomment Hapa Nchini.