November 5, 2015

NEWS: MASANJA MKANDAMIZAJI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA LUDEWA.

Masanja Mkandamizaji.

Msanii maarufu wa nyimbo za Injili na mwigizaji Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji, ameahidi kuvaa viatu vya Deo H. Filikunjombe kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Ludewa na kusema ana uwezo mkubwa na kasi kama ya marehemu Filikunjombe ambaye alikuwa rafiki yake.

Ameyasema hayo alipokuja kuchukua fomu ya kugombea kupata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi,jumla ya watu tisa akiwemo mdogo wa marehemu Fillipo Filikunjombe ambaye ni mwanasheria wa TCRA wamechukua fomu ili kuweza kuomba ridhaa.