• Isikupite Hii

  November 18, 2015

  NEWS: WAKUTWA HAI BAADA YA KUFUKIWA MGODINI SIKU 41. (+VIDEO)

  Mmoja wa watu ambao walifukiwa 

  Wachimbaji wadogo sita waliofukiwa katika mgodi mdogo wa Nyangalata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, wamekutwa wakiwa hai na mmoja kufariki baada ya kukaa chini ya ardhi kwa muda wa siku 41. Aliyefariki ni Musa supana na waliokutwa wakiwa hai ni Muhangwa Amos, Joseph Bulule, Chacha Wambura, Msafiri Gerald, Onyiwa Aido ambao wote wamelazwa katika hospitali ya kahama.

  Mmoja wa watu ambao walifukiwa na wametoka hai alisema “tulikuwa tumebaki watu sita chini, tukawa tunakunywa maji tuliyoyakanyaga na kuyakojolea, tulikula magome ya miti, mende pamoja na vyura” 

  Wenyeji wa eneo hilo wamesema walikuwa kwenye jitihada za kuitoa miili ya watu hao kutoka ndani ya machimbo ambapo walihisi kwamba wamefariki, ila baadae wakagundua kwamba kuna watu walionasa chini, ikabidi waanze taratibu za kuwatoa, wakawakuta wakiwa hai huku wakiwa na upungufu mkubwa wa maji mwilini pamoja na majeraha.
  Source: Mwananchi & MillardAyo.