January 1, 2016

MOTO UMEWAZUKIA GHAFLA WAKATI WAKIUSUBIRI MWAKA MPYA (+VIDEO)


Wakati unahesabu dakika chache kuuvuka mwaka 2015 salama, wengine wakiwa kwenye nyumba za ibada wanamshukuru MUNGU, wengine wamekusanyika na ndugu jamaa na marafiki kwa utulivu kuenjoy huku wakisubiri na kuzihesabu kwa pamoja zile sekunde za mwisho za mwaka 2015 kwa amani kabisa, iliifikia taarifa kutoka Dubai kwamba jengo moja la Hoteli limewaka moto ghafla.

Moto umeonekana kuwaka kwenye jengo la ghorofa lenye urefu wa mita 300 ambalo liko jirani na jengo refu la Dubai, Burj Khalifa huku watu wengi wakikusanyika kushuhudia tukio hilo.

Taarifa za mwanzo zimesema watu 16 ni majeruhi, vikosi vya zimamoto vimefanya kazi yao pia kuudhibiti japo chanzo cha moto hakijafahamika.

Tazama Video Hapa Chini. By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.