December 18, 2015

KIDUM AKANUSHA TAARIFA ZA KUWA AMEOKOKA, AELEZA KUHUSU PICHA ZA KUBATIZWA ZILIZOSAMBAA.


Wiki chache zilizopita kuna picha za muimbaji wa Burundi, Kidum zikimuonesha akibatizwa kwenye maji mengi zilisambaa mtandaoni na ikasemekana kuwa ameokoka na kuachana na muziki wa kidunia.

Mwanamuziki huyo mwenye makazi nchini Kenya, amefafanua kuhusu picha hizo kuwa alikuwa akishoot video mpya.

Sikudanganyi, picha zile muliona ni za video, nilikuwa nashoot video ya wimbo unaitwa ‘Mbingu na Dunia’. alisema Kidum kupitia Amplifaya ya Clouds Fm. “Sasa jamaa alikuwa anashoot video akakuwa overexcited akaweka picha zile kwa mitandao, na kujaribu kutengeneza maneno yaliyoleta hali ya sitofahamu tena bila kuniuliza. Mimi nilibatizwa kitambo sana miaka 26 iliyopita…halafu ni ukweli mi naimbaga nyimbo za injili na nyimbo za kawaida sasa ukweli ndo huo. “ alisema Kidum.

Aliendelea kusema, “Watu wenyewe wanajaribu kujulisha uma kwamba mimi nimeokoka, wanajaribu sasa kufanya nionekane muongo hata vile nilikuwa naimba nyimbo za kitambo za Kikristo kama siko mkristo, nilikuwa nadanganya ambayo silichukulii vizuri hilo neno, mimi niko mkristo na ninaishi kikristo na nimekuwa miaka mingi kwa ukristo na ninaimbaga gospel kabisa hata kuliko wale nyie mnadhani wameokoka"

Kidum amemaliza kwa kusema kuwa anaendelea kufanya muziki aliokuwa akifanya miaka yote.

“Kama kawaida vile vile naimba gospel na inspiration, mi naimbaga nyimbo za inspiration, siimbagi nyimbo za biashara biashara sana, nyimbo zangu mimi ni inspiration.”  alisema Kidum.