December 30, 2015

NGOJA-NIKUJUZE: MBWA ALIYEUAWA PARIS KUPEWA NISHANI YA USHUJAA.


Mbwa wa polisi aliyeuawa wakati wa msako baada ya mashambulio ya Paris atatunukiwa nishani kuu ya ushujaa.

Diesel, mbwa aina ya Belgian Shepherd mwenye umri wa miaka saba, alifariki wakati wa operesheni ya kumsaka mshukiwa mkuu wa mashambulio hayo.

Mbwa huyo atatunukiwa nishani kwa jina Dickin Medal ambayo hutolewa na shirika la kuwatunza wanyama la PDSA. Hadhi yake ni sawa na nishani ya Msalaba wa Victoria inayopewa watu mashujaa vitani.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.