Featured Posts

December 17, 2015

KANISA KUANDAA IBADA YA STAR WARS.


Kanisa moja mjini Berlin limetangaza kwamba litaandaa ibada maalum kabla ya Krismasi itakayoongozwa na filamu ya Star Wars.

Kuna msisimko mkubwa Ujerumani kabla ya kuzinduliwa nchini humo kwa filamu mpya ya mwendelezo wa filamu za Stars Wars kwa jina The Force Awakens Alhamisi.

Kanisa la Zion Church, lililoko eneo la katikati mwa jiji la Mitte, limetumia msisimko huo kuandaa ibada ya kipekee ya Jumapili asubuhi.

Ibada hiyo itaongozwa na filamu nambari nne ya Star Wars kwa jina Return of the Jedi.

Filamu hiyo ilizinduliwa mwaka 1983, na wale watakaohudhuria ibada hiyo wataonyesha sehemu za filamu hiyo.