December 29, 2015

GONORRHOEA KUTOTIBAKA SIKU ZA USONI - DOCTOR DAME SALLY DAVIES.


Gonorrhoea ipo kwenye hati hati ya kushindwa kutibika siku za usoni, kwa mujibu wa daktari mashuhuri wa nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa daktari huyo, Dame Sally Davies ugonjwa huo sasa hautibiki tena kwa antibiotic ya azithromycin ambapo ripoti za wagonjwa walioathirika zimeripotiwa huko Macclesfield, Oldham na Scunthorpe.

Amesema Gonorrhoea imeendelea kuwa king’ang’anizi kwa antibiotics nyingi mpya. Mwaka jana pekee watu 35,000 waliripotiwa kuugua ugonjwa huo nchini humo.


Source: dailymail.co.uk

By Chief Hope

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.