December 12, 2015

WAZIRI MKUU ABEBWA NA KUTOLEWA NJE YA BUNGE. (+VIDEO)


Bunge la Jamuhuri ya Muungano Tanzania litaanza muda sio mrefu baada ya Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 2015 kukamilika… kuna mambo ya kujibizana kwa hoja, hiyo ni kawaida… lakini kuna wakati tulishuhudia mambo yakibadilika, utata unaibuka watu wanajibizana mpaka wanataka kushikana !!

Ugomvi ni kitu kingine ambacho kimewahi kushuhudiwa kwenye Mabunge mengi, ninayo hii ya Ukraine… Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseny Yatsenyuk alikuwa amesimama mbele akiendelea na kuhutubia Bunge, Mbunge mmoja wa upinzani akamfuata na kumpa shada la maua.


Basi ile baada ya Waziri Mkuu kupokea tu hilo shada, jamaa alimbeba juujuu na kumwondoa kama anampeleka nje ya Bunge hivi… utata ukaanzia hapo, malumbano yakaendelea huku Wabunge wa chama tawala wakimgeuzia kibao Mbunge huyo na kuanza kumpiga.

Video ya tukio zima hii hapa, na imetokea leoleo December 11 2015.