• Isikupite Hii

  January 29, 2016

  NEWS:KUNGUNI NA JESHI UGANDA

   BED BUGS
  Mwandishi wa BBC Patience Atuhaire katika mji mkuu wa Uganda, Kampala amesema kuwa wanajeshi watakwenda kila nyumba kunyunyiza dawa ya kuangamiza kunguni ikiwa ni miongoni mwa shughuli zao za kijamii wakati wa kuadhimisha wiki ya jeshi.

  Kulingana na gazeti la the New Vision, wadudu hao wamejazana katika kijiji kimoja cha mabanda nje ya mji wa Kampala.

  Wiki hiyo ya jeshi ambayo huadhimishwa kila mwaka inalipa fursa jeshi kushiriki katika shughuli za kijamii kama vile kufagia barabara na kufungua mitaru ya maji taka.

  Ripota wetu amesema kuwa ni miongoni mwa shughuli za jeshi ili kujiweka karibu na raia wa Uganda.

  Source:bbc
   

  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.