• Isikupite Hii

  January 23, 2016

  LEO KATIKA HISTORIA: MAHTMA GANDHI ALIANZA HARAKATI ZA KUIKOMBOA INDIA

  http://timheaven.blogspot.com/


  Kulianza harakati kubwa ya uasi iliyoongozwa na kiongozi wa mapambano ya uhuru nchini India Mahatma Gandhi.

  Harakati hiyo kubwa ambayo iliwashirikisha wazalendo na wapigania uhuru wa India, ilifanyika kwa shabaha ya kukabiliana na maamuzi mapya ya serikali ya kikoloni ya Uingereza kuhusu ongezeko la ushuru wa chumvi.

  Katika kukabiliana na sheria hiyo ya kidhalimu, Gandhi na wenzake elfu 78 walianza kutayarisha chumvi kutoka maji ya baharini. Wakoloni wa Uingereza walikabiliana na harakati hiyo kwa kukamata makumi ya maelfu ya Wahindi na kuwatia korokoroni.

  Hali hiyo ilisababisha matatizo katika kusimamia shughuli za serikali. Mapambano hayo ya Mahatma Gandhi yaliilazimisha serikali ya kikoloni ya Uingereza kusalimu amri na kulegeza misimamo yake.


  Angalia picha za MAHTMA GANDHI hapa. Bofya hapa

  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.