• Isikupite Hii

  January 18, 2016

  MWANAMUZIKI MAARUFU WA MUZIKI WA INJILI AFARIKI DUNIA.


  Mwimbaji nyota wa muziki wa injili kutoka jamhuri ya Kidemokrasia  Kongo aitwaye Marie Misamu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. 

  Taarifa za awali zinasema mwimbaji huyo aliyetokea kupendwa nchini humo na hata baadhi ya kazi zake kupatikana nchini Tanzania, alikuwa mgonjwa (Asthma Attack) na kulikuwepo na ombi kutoka kwa bintiye aitwaye Ruth Misamu aliyewataka watu waliokuwa wakiulizia hali ya mwimbaji huyo kuwaomba wamuombee mama yake. Tutakujulisha endapo tutapata taarifa zaidi juu ya kifo chake.

  Source: GospelKitaa 

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.