January 26, 2016

BAHATI WA KENYA ATANGAZA KUACHANA NA MUZIKI WA GOSPEL.Muimbaji wa muziki wa gospel nchini Kenya, Bahati ameachana na muziki huo.

Akiongea na Pulse, Bahati alisema ameaona ni vyema akaachana na muziki huo mapema kabla ya mambo mabaya zaidi kumtokea. Alidai kuwa wasanii wenzake wamekuwa wakimpiga vita kubwa.

“Nimeamua kuachana na muziki wa gospel kwa sasa. Nimeamua kuufuata moyo wangu. Wasanii wa gospel, kaka zangu, wamekuwa wakikutana kisiri kupanga anguko langu. Nina maumivu makali moyoni mwangu. Haina faida kuwa kwenye tasnia ya gospel tena,” alisema.

“Katika kiwango hiki, chuki hii inaweza hata kuniua. Kama wanaweza kwenda mbali zaidi kwa kutafuta ndugui zangu na watu wengine walio karibu na mimi kuwapa rushwa na kuwataka watunge uongo dhidi yangu, unadhani hawawezi kufanya chochote kunimaliza?”

Hadi sasa Bahati amefuta picha zote alizowahi kupost kwenye mitandao ya kijamii.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.