• Isikupite Hii

  January 27, 2016

  BASATA YAWATAKA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUJISAJILI.


  BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limezidi kutoa wito kwa Waimbaji wa muziki wa Injili kujisajili katika baraza hilo ili stahiki zao zitambulike inavyotakiwa.

  Mkurugenzi wa ukuzaji Sanaa na Mtukio wa Basata, Maregesi Kwirujira Ng’oko alisema waimbaji wengi wa muziki wa Injili wa Tanzania kuzingatia hilo. 

  Ng’oko alisema kujisajili Basata kuna faida na fursa nyingi ambazo ni msaada ambao utasaidia kupata haki zao kupitia kazi zao. 

  Ng’oko alisema kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa kazi za sanaa ni jukumu lao kuwakumbusha mara kwa mara wasanii kujisajili. 

  Aidha Ng’oko alisema wanatoa salamu hizo kwa wasanii pindi inapotokea mikinzano katika ufanikishaji wa kazi zao. 

  Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era alisema wanafikiria kuongeza msukumo kwa waimbaji wa muziki wa Injili kuhusu kujisajili Basata katika baadhi ya matukio. 

  Mang’era alisema wanafikiria kutoa elimu ya kujisajili BASATA katika matamasha yao ama kusaka namna ya kufanikisha utambuzi wa waimbaji katika baraza hilo.
  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984.Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini 

  Dira Kuwa chombo chenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa huduma bora kitaifa katika maendeleo ya sanaa 

  Lengo kuu Kufufua, kukuza na kuongeza maendeleo ya utengenezaji wa kazi bora za sanaa. 

  Maadili Maadili ya msingi ya Baraza la Sanaa la Taifa ni kuhimiza na kukukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania, kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu na kuchochea ubunifu na uvumbuzi katika sanaa.
  • Limepania kuhimiza na kukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania
  • Limepania kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu
  • Limepania kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika sana


  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.